Na Mwandishi Wetu
Watanzania wamethibitisha kwa kuonyesha dhahiri mwitikio mkubwa katika kampeni za uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi CCM kwa kusema hawatapoteza bahati na lulu iliyopo kwa kuendekeza hongo za mabeberu.
Lulu ya Tanzania ambayo sio rahisi kupatikana mahali popote duniani na wapo watu wengi katika nchi nyingine ambapo wanatamani usiku na mchana Mungu angewasaidia wakampata kiongozi wa Tanzania angalau kwa miezi mitatu tu ili wafaidike na mchakamchaka wa maendeleo unaoendelea katika nchi ya Tanzania.
Nini maana yake unaposikia watu wa nchi mbalimbali wanatamani kiongozi wenu angekuwa kiongozi wao awaongoze hata kwa muda mfupi tu ili mradi wapate taratibu zake za kufanya kazi, kiuadilifu, kwa moyo mmoja na kuwapatia maendeleo wananchi wa hali ya chini yaani wanyonge?.
Moja ya chombo cha habari maarufu nchini Nigeria kilimtaja Rais Magufuli kuwa ndiye Rais bora kwa sasa Barani Afrika na kuanza kutaja mambo mbalimbali ambayo ameyafanya na anaendelea kuyafanya na kusema kuwa wana hakika hivi karibuni Tanzania itakuwa nchi bora na kuachana na hadithi za umasikini, ambapo utabiri huu umetimia ndani ya miaka mitano ambapo Tanzania imetoka uchumi wa chini na kuingia uchumi wa kati kabla ya muda uliotarajiwa wa mwaka 2025.
Adeola Fayehun channel ambayo ni maarufu sana nchini Nigeria ni mojawapo inayotangaza utendaji wa Rais Magufuli kwa Wanigeria ambao wanatamani Rais Magufuli angekuwa Rais wao. Channel hiyo imethibitisha jinsi Waganda na watu wa Afrika ya Kusini wanatamani Rais Magufuli angekuwa kiongozi wao.
Watanzania hili si jambo dogo na si kila Rais anayetawala nchi fulani watu wanataka awe kiongozi wao. Hapa kuna fumbo kubwa la kujiuliza kwa nini Rais Magufuli?.
Mnamo tarehe 17, Aprili, 2019 Rais Magufuli alifanya ziara Mkoa wa Ruvuma na alitembelea barabara ya Mbinga na kuwataka wakandarasi kutoka China wanaojenga barabara ya Mbinga Mbamba Bay wamalize haraka barabara hiyo kabla ya mwaka 2020 na hapa mmoja wa Raia wa Afrika ya Kusini akaandika katika mtandao wa kijamii ,
“Chucicco Cimama Can u borrow us this president in South Afrika plz we need him agently” Mnaweza kutuazima Rais huyu hapa Afrika ya Kusini tunamhitaji kwa udi na uvumba “
Katika mada hiyo Sun Kem ameandika This man is a hard working man, he knows what work is and nobody can fool him easily. Ambapo Tosh Di Don ameandika We need you here in our small Gambia, Naye Man of Reality amesema am kenyan bt prez magufuli is my prsdnt, haikuishia hapo huyu String Master ameandika Tanzania please send him to Cameroon and we give you Paul Boyar just for two yrs. Thanks for understanding. Naye Preston Chakai ametoa mawazo yake na kuandika The hardworking president of Africa Naye Sare King amesema Wow we love u from nigeria, If every president is like u the all Africa could have been a better place. God bless you sir.
Ukitaja jina la Rais Magufuli mwenye fikra za kuhakikisha nchi yake inajilisha kwa kuzalisha chakula bila kuwa ombaomba, kushiriki katika miradi mikubwa na kupata suluhisho la changamoto mbalimbali zilizokuwepo. Rais amekuwa kinara katika ukuaji wa uchumi wa nchi ya Tanzania ambapo mchakamchaka wa maendeleo aliouendesha, matokeo yake yameonekana kwa kila Mtanzania mpenda maendeleo.
Aidha, Rais Magufuli amethubutu kufanya kila anachofikiri na kukiweka katika utekelezaji, mengi yamefanywa na Rais huyu ambayo yote yalikuwa ndoto ya kusadikika kwa kuwa haikuwa rahisi kwa Mtanzania wa kawaida kuamini kuwa kitendawili cha mafanikio hayo yaliyokuwa anayaota yanaweza yakafanyika. Uthubutu wake wa kupambana na mabeberu unazidi kudhihirika duniani kama alivyopambana na suala la madini na kuhakikisha suala la kuiba rasilimali za Tanzania linakuwa hadithi za kusadikika.
Rais Magufuli akiwaangalia mabeberu anaona ushindi kwa kuwa ameweza kutekeleza wazo la Baba wa Taifa Julius Kambarege Nyerere la ujenzi wa miradi mikubwa kama bwawa la Nyerere (Stigler’s Gorge). Mradi huu ni tishio kwa mabeberu kwa kuwa wanaona Tanzania ya viwanda imefanikiwa. Amevunja rekodi kwa kuhakikisha yale yote aliyoyaweka kimaandishi au kwa maneno kutoka Mwalimu Nyerere ameyaweka katika utekelezaji ikiwa ni ahadi yake ya kuwatumikia wananchi wanyonge wa Tanzania, kuondoa umaskini na kuhakikisha Taifa la Tanzania linakuwa kiuchumi na kufikia uchumi wa kati 2025 ajabu ahadi ambayo ameitimiza kabla ya mwaka uliokusudiwa.
Rais Magufuli ameweza kufufua vita ya uchumi ambayo mchakamchaka wake unawashangaza na kuwabakiza midomo wazi wezi, wanyonyaji makabaila na mabwanyenye ambao kila kuchwea wanatafuta mbinu mpya za kuziba ubongo wake kufikiri na kufanya kazi. Afrika inaweza kujilisha, kujinywesha, kujisitiri, hakuna haja ya kwenda kwa wazungu ndio maana haoni umuhimu wa kwenda Ulaya wakati wapo mabalozi kila sehemu ambao amewateua kwa ajili ya kufanyia kazi Tanzaia sasa yeye aende Ulaya kufanya nini au ni suala la ubadhilifu wa fedha za umma?.
Ujasiri wa Rais Magufuli ni kama wa Nyerere pale Baba wa Taifa alipowatimua wale Waswidishi waliokataa Tanzania kupata asilimia 51 na wao kupata asilimia 49 katika mradi wa dhahabu wa Bulyankulu Shinyanga ambapo walikataa na mradi huo kusimama na Mwalimu akasema “uzuri dhahabu haiozi tutaichimba pale tutakapokuwa na uwezo wa kufanya hivyo”
Magufuli amesema ni aibu sisi kama Waafrika kutembeza bakuli na kuwa ombaomba kwa wazungu wakati sisi tunacho kila kitu
Akihutubia Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika-SADC , ambapo Rais alikabidhiwa uenyekiti alisema “Afrika sio masikini nchi zetu ni tajiri kwa sababu malighafi zote zinatoka Barani Afrika kwa nini sasa tunashindwa kutumia rasilimali tulizo nazo kwa ajili ya kujiletea maendeleo yetu wenyewe?”
Ushuuda upo baadhi ya Marais wa nchi mbalimbali wametuma watu wao kuja kujifunza mambo mbalimbali ambayo Rais Magufuli ameonyesha mfano wa kuigwa kama vile Afrika ya Kusini kuja kujifunza masuala ya Madini Uganda pia imefanya hivyo. Aidha Rais wa Burundi Evariste Ndayishime amethihirisha kuwa Tanzania ni sehemu sahihi ya kujifunza mbinu mbalimbali za kuinua uchumi wao na kumuomba Rais Magufuli katika hili asimuache abaki nyuma kwa kuwaruhusu Warundi waje wauze madini yao katika soko la madini Mkoa wa Kigoma ambapo wataweza kupima ubora wa madini husika.
Pia, tumeona ziara ya Rais wa Malawi nchini Tanzania Dkt Lazarus Chakwera hivi karibuni ameweza kumuaomba Rais aweze kushirikiana naye ili aige mambo kadhaa ambayo anaona akiwa sambamba naye na Malawi itajikomboa kiuchumi
Rais Mstaafu wa Nigeria Dkt. Elusegun Obasanjo amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya katika uongozi wake ikiwemo kupambana na rushwa, kuimarisha utoaji wa elimu, kuimarisha miundombinu, kuongeza nishati ya umeme, kuboresha usafiri wa ardhini na angani na jinsi wadau mbalimbali wa ndani na nje wanavyopaswa kuelewa juhudi zinazofanyika. Jiulize unawezaje kuacha Lulu uliyonayo kwa Hongo za Mabeberu?.
Yapo mambo muhimu ambayo ameyafanya Rais huyu na kuwapiga vikumbo mabeberu na kamwe Watanzania hawawezi kuiacha ‘Lulu yao kwa hongo za Mabeberu’ kama vile, vituo vya Afya vimeongezeka kama uyoga nchi nzima, utoaji wa elimu bure iliyogharimu Trilioni 1,158,583,516,691 na Tanzania kuwa kinara katika nchi za Afrika kusambaza umeme vijijini uliogharimu bilioni 990,500,000,000 kwa nchi nzima umeme umefikia asilimia 80. Barabara za lami kila Mkoa, Wilaya madaraja ya juu, kama vile Fly Over TAZARA na Ubungo) barabara 8 Dar-es-Salaam -Kibaha, ujenzi wa meli na vivuko katika Maziwa Makuu imegharimu bilioni 152,000,000,000 upanuzi wa viwanja wa ndege ikiwemo terminal 3, ulinzi wa madini yetu na ujenzi wa ukuta wa Mererani ambapo matokeo yake imezalisha mabilionea wa Kitanzania.
Suala la zima la kujizatiti katika kuboresa huduma za jamii, ikiwemo maji na kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata mikopo ya elimu ya juu ni ushahidi tosha wa kudhamiria kuondoa umasikini, ujinga na maradhi maadui watatu wakubwa ambao Baba wa Taifa la Tanzania alipambana nao. Utekelezaji wa ujenzi wa mradi mkubwa wa reli ya kisasa ya SGR ni kielelezo muhimu katika kukuza uchumi wa Tanzania na hili sio siri ni kikumbo kingine cha kishindo kwa Mabeberu wamebaki wanaweweseka usiku na mchana wakitaka jambo hili likwame ili waweze kuwateka vizuri Watanzania na kufaidi uchumi wao.
Hulka ya kiongozi wa Tanzania anayemtanguliza Mungu, katika kila jambo alifanyalo iliwapa nguvu wananchi na kutochanganyikiwa wakati wa janga la ugonjwa wa Covid-19. Utafiti wa makini kuhusu sampuli zilizopelekwa Maabara ya Taifa na kutoa matokeo yanayotatanisha ni ushahidi uliomfanya Rais Magufuli kuwa na msimamo kuhusu ugonjwa mzima wa Covid-19 na kuwa na mjadala mpana katika mitandao ya kijamii.
Katika mitandao ya kijamii baadhi ya watu mbalimbali duniani wanaongea nini kuhusu matamshi yake:
I’m from Kenya, na namkubali Magufuli sio fisadi kama hapa kwetu, he puts Tanzania first, this is a good example of a true leader, mumuache huyu bwana aongoze Tanzania hata miaka 20, hamna haja ya Siasa kila wakati,,, hongera 255
Haikuishia hapo hata shirika kubwa duniani lilidhubutu kuikosoa Tanzania lakini mbio za sakafuni huishia ukingoni huwezi kushindana na Mwenyezi Mungu hata siku moja. Shirika hilo liliikosoa Tanzania kupitia kiongozi wake mwandamizi aliikosoa Tanzania kwa kuchelewa kuchukua hatua za mapema kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo. Mnamo Tarehe 24 Aprili Mkuu wa WHO wa Bara la Afrika Bi Matshidiso Moeti alisema kumekuwa na hofu juu ya kukua kwa kasi ya maambukizi katika taifa hilo la Afrika Mashariki.
“Kwa hakika tumeona kuwa watu kuacha kutangamana, pamoja na kupiga marufuku kwa mikusanyiko ya watu wengi kumechukua muda mrefu kufanyika na tunaamini kuwa hayo yanaweza kuwa ni moja ya mambo yaliyosababisha ongezeko la kasi la wagonjwa wa corona,” alisema Dkt Moeti katika mkutano na wanahabari.
Rais Magufuli alisema “Wapo wengine wanatoa mawazo ya kuifunga Dar es Salaam, hili haliwezekani. Dar es salam ndio centre (sehemu) pekee ambapo collection (makusanyo) ya revenue (mapato) inapatikana kwa nchi yetu. Zaidi ya asilimia 80 ya mapato yanakusanywa Dar es Salaam,”
Pamoja na yote hayo Rais alichukua hatua kadhaa ambazo zilitekelezwa na pale utafiti wake makini ulipokamilika, aliweza kutoa uamuzi wenye busara kwa kukabidhi suala la Corona kwa Mwenyezi Mungu. Ambapo athari za kuwafungia watu lilikuwa ni janga la Taifa na maamuzi yake yakaweza kuungwa mkono na mataifa mengi makubwa duniani ambao wamechelewa kutoa maamuzi sahihi katika kuwalinda raia wao.
Yapo masuala mengi ambayo kamwe Watanzania hawawezi kukubali kuiacha Lulu yao kwa Hongo za Mabeberu ni kama vile kujifadhili kwa Tanzania katika Bajeti yote ya uchaguzi mwaka 2020 ambapo wengi wamejiuliza kuna maana gani? Jambo hili limeishangaza dunia kwa Tanzania kutoa zaidi ya shilingi bilioni 300 kwa ajili ya mchakato wa uchaguzi uweze kufanyika kama ilivyokusudiwa. Hapa ndipo vyombo mbalimbali vya habari vikataka kujua hii ina maana gani kwa Tanzania kujifadhili katika Bajeti yote ya uchaguzi kupitia mtandao wa kijamii wa BBC
Hassan Ismail ameandika Tanzania kujifadhili katika Bajeti ya uchaguzi ina maana nchi imebadilika itafikia wakati tutapunguza utegemezi ndio maana kura yangu kwa Mh. Magufuli tano tena nchi imebadilika miundombinu na mengine mengi .Mh. Magufuli Mwenyezi Mungu akupe afya njema.
David Jackson amesema maana yeke ni kwamba Tanzania sasa inaweza kujisimamia na kuendesha mambo yake ya ndani ya nchi bila kubughudhiwa na ukiona hivyo jua uchumi wake uko imara.
Naye Nassir De Santos Mohammed ameandika “pesa ipo pia madeni ya wazungu yana athari sana kiuchumi kwa sababu ya riba kubwa, hapo ndio ninapompa credit JPM Serikali yake haikopi kizembezembe miradi mingi anaiendesha kwa pesa ya ndani”.
Deogratius Ngowi amesema kuondoka na kupangiwa nani awe madarakani pia kuondokana na madhila ya kugawa rasilimali zetu ili watufadhili fedha zao hivyo kama taifa huru ni vema kwa Taifa letu kutoa fedha za walipa kodi kwenye uchaguzi kuliko kupewa vya bure vinaua. Paulo Massawe ameandika kuna maana kubwa sana kwani misaada sio yote hutolewa kwa nia njema tufike pahala ata sisi tuwape wao msaada.
Jackson ameandika ni Hatua nzuri ya JPM kujenga misingi ya kujitegemea kama taifa na kuondokana na dhana ya utegemezi. Najua wazungu hawapendi maana kidogo kidogo tunajiondoa kwenye makucha yao ndio maana sasa wanatumia vibaraka wao kupinga kila kitu.
John Eljih Nimepanda sana kutoa fedha zetu wenyewe tutategemea misaada mpaka lini , tuanze kujitegea wenyewe sasa tumeanza na hili na vingine vitafuata. Upendo John maneandika Ndio mjue Rais Magufuli hayumbishwi kizembezembe anajielewa mikopo nayo ni sehemu ya utumwa . Pia, huishia kuweka nchi rehani na raia wake Tanzania tunakwenda na Magufuli wetu hatukurupuki 5 tena kwa Magufuli wabunge CCM na Madiwani.
Asha Juma ameandika Tumekuwa kiuchumi na tunaweza kujitegemea kwa kiasi Fulani huo ni mwanzo mzuri , tunaimani miaka ijayo tunaweza kufanya mengi makubwa na kusimama wenyewe Mungu Ibariki Tanzania.
HAKIKA HATUWEZI KUIACHA LULU YETU KWA HONGO ZA MABEBERU.