…………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, MWANZA
Mabingwa wa kihistoria Tanzania timu ya Yanga imeendelea wimbi la ushindi Ligi Kuu Vodacom baada ya kutoka nyuma na kushinda mabao 2-1 dhidi ya wenyeji wahamiaji, KMC Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Mchezo ulianza kwa kasi na dakika ya 27 wenyeji KMC walipata bao la kuongoza lililofungwa na winga machachari Salum Kabunda akipokea pasi ya Kenny Ally Mwambungu.
Yanga walisawazisha bao hilo kupitia kwa winga wao hatari TK Master Tuisila Kisinda kwa mkwaju mzuri wa penalti dakika ya 41 akimchambua kipa mkongwe Juma Kaseja kufuatia mshambuliaji Mghana, Michael Sarpong kuangushwa kwenye boksi.
Shujaa wa Yanga alikuwa mshambuliaji wake mpya, Waziri Junior aliyemalizia kwa kichwa kona ya Farid Mussa Malik dakika ya 61.
Baada ya kufunga bao hilo, Waziri, alivua jezi kuonyesha fulana iliyoandikwa “The King of CC Kirumba Stadium’, akimaanisha yeye ni Mfalme wa Uwanja huo kutokana na rekodi yake ya mabao tangu akiwa anachezea Toto Africans na Mbao FC zote za Mwanza ambazo zimeshuka Daraja.

Kwa ushindi huo, Yanga imefikisha pointi 19 katika mchezo saba na wanendelea kubaki nafasi ya pili, nyuma ya vinara, Azam FC waliokusanya pointi zote 21 katika mechi saba wakati mabingwa watetezi,Simba SC ni wa tatu kwa pointi zao 13 za mechi sita.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo; Biashara United imeshinda 1-0 dhidi ya wenyeji, Polisi Tanzania bao pekee la Deogratius Judika Mafie dakika ya 53 Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.
JKT Tanzania ikaichapa 6-1 Mwadui FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga mabao ya timu ya Jeshi la Kujenga Taifa yakifungwa na Adam Adam matatu dakika ya 24, 48 na 82, Danny Lyanga dakika ya 40 na 52 na Said Luyaya dakika ya 90 na ushei, wakati la wenyeji limefungwa na Pastory Athanas dakika ya 62.
Ligi Kuu itaendelea kesho kwa mechi tatu, ikiwemo mabingwa watetezi, Simba SC kumenyana na Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Dodoma Jiji na Tanzania Prisons Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na Mtibwa Sugar na Azam FC Uwanja wa CCM Gairo, Dodoma.