Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia mkutano wa Ufungaji wa kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM kwa Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na Wananchi wa Unguja katika Uwanja wa Demokrasia Kibanda Maiti Zanzibar leo Octoba 25,2020.
Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mgombea kiti cha Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya cha Mapinduzi CCM Dkt. Hussein Mwinyi alipowasili katika uwanja wa demokrasia Kibanda Maiti Zanzibar kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Ufungaji wa kampeni za Chama cha Mapinduzi CCM leo Octoba 25,2020.
Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM na Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kwenye mkutano wa ufungaji wa kampeni za CCM katika Uwanja wa Demoktrasia Kibanda Maiti leo Octoba 25,2020. kulia nia Mgombea kiti cha Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya cha Mapinduzi CCM Dkt. Hussein Mwinyi.
*************************************
IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk.Hussein Ali Mwinyi alisema akichaguliwa kuwa rais atakipa hadhi maalum kisiwa cha Pemba ya kuwa eneo la uwekezaji ili kiende sambamba kimaendeleo na kisiwa cha Unguja.
Ahadi hiyo aliitoa wakati akihutubia katika ufungaji wa kampeni za CCM za uchaguzi mkuu wa dola wa mwaka huu,huko katika viwanja vya demokrasia kibanda maiti Unguja.
Alisema wakati umefika wa Wananchi kumchagua rais aliyezaliwa baada ya mapinduzi ili alete mapinduzi makubwa ya kiuchumi nchini.
Alisema anaomba kura nyingi za ndio ili aweze kuwatumikia na kuleta matumaini makubwa ya kimaendeleo.
Alisema licha ya kuzaliwa baada ya mapinduzi lakini anaifahamu historian ya Zanzibar,ambayo waasisi waliikomboa kutoka katika mikono ya utawala wa kigeni.
Alisema mapinduzi hayo ya mwaka 1964 ndio chanzo cha maendeleo yaliyopo hivi sasa.
Akizungumzia muungano alisema ni chimbuko la maendeleo na kwamba wanaobeza muungano wapuuzwe kwani hawana sera zenye tija.
Alisema kwamba ataimarisha uchumi mpya wa Zanzibar kupitia sera ya uchumi wa buluu uliobeba sekta nyingi za maendeleo.
Alisema atawaendeleza kwa kuwapa mikopo wavuvi ili wanunue dhana za kisasa ili wafanye uvuvi wenye tija.
Alisema atawaondoshea wafanyabiashara vikwazo vinavyokwamisha kufanya biashara zao kutokana na uwepo wa Kodi nyingi.
Alisema katika ukuaji wa kiuchumi ni lazima kujengwe miundombinu ya kisasa ya barabara za viwango vya lami.
Alisema ataimarisha miundombinu ya umeme na kuwapunguzia gharama za umeme wananchi wenyewe kipato cha chini.
Alisema ataimarisha shirika la umeme ili lijiendeshe lenyewe kibiashara.
Alisema katika juhudi za kukuza uchumi wa nchi lazima iwepo nishati ya uhakika ya umeme ambao utatumika viwandani na katika miradi ya uwekezaji sambamba na kuanzisha nishati mbadala za umeme wa jua.
Alisema ataimarisha sekta ya mafuta na gesi ili mafuta hayo yachimbwe na kuwanufaisha wananchi.
Alisema kwamba atajenga hospitali kubwa ya rufaa itakayokuwa na uwezo wa kutoa huduma ya upasuaji wa moyo.
Alisema atajenga vituo 32 vya huduma za mama na mtoto ili vitoe huduma kwa masaa 24.
Ataendeleza kujenga hospitali kubwa ya Binguni ambayo itatoa huduma bora na zenye viwango.
Atazipatia vifaa vya kisasa na ziwe na hadhi ya hospitali za wilaya hospitali za Kivunge na Makunduchi.
Alisema katika kujenga uchumi wa Zanzibar ni lazima kuwashirikisha wadau wa maendeleo.
Aliwakaribisha wawekezaji wa nje na wenyeji,watanzania wanaishi nje kuja kuwekeza nchini.
Alisema ataweka sera na sheria nzuri za kusimamia uwekezaji ili kuwavutia watu wenye nia kuja kuweza nchini.
Alisema ili kufikia malengo hayo ni lazima kuwepo na utawala bora huku akiwawajibisha wazembe na wala rushwa.
“Kuna watu wanasema mimi ni mpole lakini upole wangu sio udhaifu na nasema kuwa watanielewa.”,alisema Dk.Mwinyi.
Katika sekta ya uwezeshaji alisema atawapatia mafunzo,mikopo na masoko wajasiriamali mbalimbali.
Alisema atawaondolea utitili wa kodi wafanyabiashara ndogo ndogo na watapewa vitambulisho maalum watakavyolipia Kodi mara moja kwa mwaka.
Alisema ataimarisha maslahi kwa watumishi wa umma kwa kuongeza mishahara yao na kuboresha maslahi ya wastaafu.
Alisema kwamba ataimarisha makundi maalum hasa vijana ambao atawapa ajira katika sekta za umma,binafsi na wengine watawezeshwa na kujiajiri wenyewe.
Alisema ataimarisha miundombinu ya barabara ambapo atajenga barabara ya Tunguu -Jumbi (km 9.3),Jozani -Charawe -Ukongoroni-Bwejuu (km 23.3), Kizimbani -Kiboje (km 7.2),Kinduni-Kichungwani-Kitope(km 3.5),Umbuji -Uroa (6.9),Mkwajuni -Kijini (km 9.4),Sharif Mussa- Mwananya-Bububu skuli(km 3.5),Fumba -Kisauni(km 12) na Tunguu Makunduchi (km 48) .
Alisema ataendeleza michezo na burudani kwa kulea makundi mbalimbali ya Sanaa na michezo ili fani hizo ziwanufaishe vijana.
Alisema kwamba atashughulikia soka la Zanzibar ili hadhi take irudi kama zamani.
Alisema atahakikisha anazuia dawa za kulevya kwa kudhibiti wasambazaji na wauzaji na wale walioathirika na dawa hizo watatibiwa katika soba.
Alisema kuwa atadhibiti vitendo vya udhalilishaji wa wanawake na watoto ili wapate haki zao kama walivyo watu wengine.
Kwa upande wake Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,amewataka wananchi wawachague wqgombea wa CCM ili waendelee kulinda tunu za mapinduzi,muungano,uhuru pamoja na amani.
Alisema kuwa wagombea wote waliosimamishwa na CCM wana sifa na vigezo vya kuwatumikia wananchi kwa uadilifu mkubwa.
Alisema kuwa CCM imendelea kuleta maendeleo kupitia usimamizi mzuri wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 iliyoleta mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali za umma na serikali.
Akizungumza Rais mstaafu wa awamu ya nne wa serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete alimpongeza rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020.
Alisema Zanzibar ya sasa sio Zanzibar aliyoipokea Dk.Shein ya mwaka 2010 kwani kwa sasa nchi imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo.
Alisema Zanzibar inang’ara kwa miundombinu ya kisasa ya barabara,umeme,kuimarika kwa huduma za kijamii pamoja na kukua kwa pato la taifa kwa kuwa na uchumi ulioimarika.
“Nikupongeze sana Dk.Shein umefanya kazi kubwa sana ya kuimarisha maendeleo ya Zanzibar, sasa nakukaribisha katika umoja wa Marais wastaafu hakika utamaliza muda wako kwa heshima kubwa”,alisema Dkt.kikwete.
Dkt.Kikwete akitaja sifa za Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa kusema kuwa ni kiongozi muaminifu na muadilifu anayechukia vitendo vya rushwa na uonevu.
Alisema kuwa amefanya kazi na Dk.Hussein kwa kipindi cha miaka 10 ambaye kila wizara aliyoihudumu alipohamishwa walikuwa wakisikitika sana kwa kutaka asiondolewe.
Alisema Dk.Hussein ni mchapakazi asiye na majivuno anayependa kufanya kazi kwa bidii kubwa.
Aliwahakikishia wananchi kuwa Dk.Hussein ndio chaguo sahihi la kuiongoza Zanzibar kwani ana sifa zote za kuipandisha Zanzibar katika kilele cha mafanikio.
Alisema kwamba sifa nyingine ya Dk.Hussein ni msomi wa fani ya udaktari hivyo kuwatumikia wananchi ni sehemu ya maisha yake.
Alisema kwamba Dk.Hussein ni mgombea bora kuliko wote aliogombea nao kutoka katika vyama vingine vya siasa Zanzibar kwani ana sifa ya uzoefu wa kiutendaji ndani ya Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Alisema anawaombea kura wagombea Uwakilishi,Wabunge na madiwani ili
waweze kusaidiana kazi za kuwatumikia wananchi.
Alisema katika kujenga Tanzania imara kiuchumi,kijamii na kisiasa ni muhimu wananchi kuwachagua wagombea urais wa jamhuri ya muungano kwa tiketi ya CCM Dkt.John Pombe Magufuli na mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk.Hussein Ali Mwinyi kwani Wana dhamira ya kuleta mapinduzi makubwa ya kimaendeleo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Nabodi,amesema CCM imefunga kampeni zake kwa kupata mafanikio makubwa ya wananchi wengi kujitokeza kusikiliza sera na mikakati ya chama hicho.
Alisema kuwa CCM Zanzibar imetekeleza kwa ufanisi maagizo ya halmashauri kuu ya CCM Taifa ambayo pamoja na mambo mengine ilielekeza uendeshaji wa kampeni za kistaarabu ili kutoa fursa pana ya kuwafikia wananchi wa makundi yote ya kijamii.
Alisema Chama Cha Mapinduzi kimeendelea kuwa karibu na wananchi kwa kuhakikisha kinaleta maendeleo endelevu.
Alisema CCM inatarajia ushindi mkubwa wa kihistoria ambao haukuwahi kutokea toka mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, kwani imetekeleza kwa ufanisi Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020.
Aliwapongeza Wana CCM wa makundi yote kwa ushiriki wao mkubwa waliotoa katika kipindi chote cha kampeni.