*****************************************
NA DENIS MLOWE,IRINGA
CHAMA cha Mapinduzi wilaya ya iringa Mjini, kimejinasibu kuibuka na
kura za kishindo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28
kwa upande wa mgombe wa Urais,wabunge na madiwani kutokana utekelezaji
wa ilani uliofanywa na serikali ya awamu ya tano.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa CCM wilaya ya iringa Mjini Said Rubeya
wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake kuwa ccm wilaya ya
Iringa na mkoa kwa ujumla wamejipanga vyema kimkakati na sababu za
ushindi wa kishindo walizonazo.
Alisema kuwa sababu mojawapo inayowafanya waibuke na kura za kishindo
kwenye chaguzi hiyo ni uwingi wa wananchama wa CCM mkoa wa Iringa
ambapo wanasababisha wawe na asilimia 41 ya kura kutokana na wanachama
zaidi ya laki moja waliopo mkoani hapa.
Aidha alisema kuwa sababu nyingine itakayosababisha ushindi wa
kishindo kwa chama hicho ni kuweka wagombea wote wanaokubalika kuanzia
ngazi ya urais, wabunge na madiwani na kutolea mfano kwa ubunge iringa
mjini kwa mgombea Jesca Msambavangu kuwa anakubalika na kila rika
katika chaguzi ya mwaka huu.
“Sisi CCM katika jimbo la iringa mjini tumejipanga vyema kabisa
kuibuka na asilimia zaidi ya 65 kwa nafasi ya ubunge asilimia 80
nafasi ya urais na asilimia 80 na nafasi ya madiwani asilimia 85 hadi
100 kutokana na kuwasimamisha wagombea wanaokubali na wapiga kura
mkoani hapa” alisema
Alisema kuwa sababu nyingine itakayosababisha kuibuka na kura za
kishindo ni wananchi kuchoshwa na uwongo , uzandiki wa wapinzani hivyo
kutoa kuwapa kura za kutosha kwa wagombea wa ccm na kuongeza kuwa
sababu nyingine ni kufilisika kisiasa kwa mbunge alioko jimbo la
Iringa mjini.
Aidha Rubeya alisema kuwa wananchi wa wilaya ya iringa wamechoka
kuongozwa na mbunge ambaye hajafanya chochote tangu kuingia kwake
madarakani hali ambayo inasababisha watakipigia kura chama cha
Mapinduzi na sababu nyingine kubwa kabisa itakayosababisha ushindi ni
kuungwa mkono na makundi mbalimbali ya wapiga kura.
Alisema kuwa wananchi sababu nyingine ya CCM kuibuka kidedea ni
wananchi wa manispaa ya Iringa kuchoshwa na siasa ya kutenganishana
na mgawannyiko unaofanywa na aliyekuwa mbunge pamoja na chama chake
cha Chadema.
“ Kwa maana hiyo sisi CCM tunaona ushindi dhahiri kabisa kwetu na
katika tafiti tulizofanya nafasi ya urais tutaibuka ana asilimia
80-85 ya wapiga kura wote 1026,108 na katika ubunge ni asilimia 65
mpaka 70 na nafasi ya udiwani katika kata kumi na nane tatupata
asilimia 88 mpaka 100.” Alisema
Alisema kuwa wamejipanga vyema na wanajivunia kazi nzuri zilivyofanywa
na Rais John Magufuli ambazo zinaonekana ikiwemo kupambana na rushwa
kwenye sekta za umma, kuboresha sekta ya afya, elimu bure, na ongezeko
la ukusanyaji wa mapato kutoka wastani wa bilioni 800 kwa mwezi hadi
trilioni 1.5 kwa mwezi.
Aliongeza kuwa serikali ya awamu ya tano imeimarisha uwekezaji wa
viwanda hali ambayo imesababisha kuwepo na zaidi viwanda vipya 8477
vikiwemo vidogo, vya kati na vikubwa vilianzishwa kipindi hiki cha
awamu ya tano na kuwezesha ajira zapatazo 482,601.