NA DENIS MLOWE,IRINGA
ALIYEKUWA mtia nia ya kugombea ubunge jimbo la Kilolo, Mugabe
Kihongosi ametoa wito kwa watanzania kuendelea kumwamini mgombe wa
CCM John Pombe Magufuli kwa kumpa kura za kishindo ili aweze
kukamilisha malengo ya kueletea maendeleo zaidi kwa kipindi cha miaka
mitano mingine.
Akizungumza na mwanahabari hizi, Kihongosi alisema kuwa kwa miaka
mitano tangu Magufuli aingie madarakani amejipambanua kwa kiasi
kikubwa kwa miradi mbalimbali mikubwa aliyofanya hivyo watanzania
wampe kura za kishindo Oktoba 28 mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu.
Kihongosi ambaye alipewa nafasi kubwa kuibuka kidedea kwenye kura za
maoni alisema kuwa kitendo cha nchi kufika uchumi wa kati kabla ya
matarajio imeonyesha ni kiasi gani rais Magufuli ametenda kazi nzuri
ambayo zawadi kubwa ni kumwongezea miaka mitano mingine kuweza
kuifikisha mbali zaidi Tanzania.
Aidha aliwataka wananchi nchini kuweza kukamilisha mafiga matatu
katika uchaguzi huo kwa kuwachagua viongozi wanaotokana na chama cha
Mapinduzi kuanzia ngazi ya udiwani, ubunge hadi urais kwani kutakuwa
na muunganikani mzuri wa kuwaletea maendeleo wananchi kwa kuwa
itatumika lugha moja ya maendeleo.
Aidha alitoa wito kwa Watanzania kuendelea kudumisha amani iliyopo
katika kuelekea uchaguzi mkuu na kuwataka vijana kuepuka kutumika
vibaya na wanasiasa wenye malengo mabaya na nchi kwani wengine
wamepanga wakishindwa kutaka kuvuruga amani na wanaotumika zaidi ni
vijana.
“Tuenzi amani ambayo baba wa Taifa alituachia sisi watanzania kwani
ndio imefanya nchi itambulike asitokee mtu akataka kuivuruga kisa
kutaka madaraka hivyo ni jukumu letu sote kuwapinga wavuruga amani wan
chi yetu” alisema
Kihongosi alisema kuwa vitu ambavyo vinaweza vuruga amani katika
uchaguzi ni watu kutozingatia utaratibu na kanuni zilizowekwa aidha na
tume ya uchaguzi na serikali kwa ujumla na kutoa rai siku ya uchaguzi
watu wajiepushe na mavazi ya vyama na kufata taratibu zilizowekwa.
Aidha alitoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama kutoa elimu na
kuepuka kutumia nguvu kubwa kwa wapiga kura kwani wenye kulinda amani
sisi watanzania na wenye kuvuruga amani ni sisi pia hivyo vijana
wajitokeze kupiga kura kwa wingi na kurejea majumbani kusubiri
matokeo.
Aliongeza kuwa kuna baadhi ya watu wanaogopa kwenda kupiga kura
wakijua kwamba kwenye uchaguzi kutakuwa na vitisho, kutakuwa na vurugu
kikubwa nawasihi nchi yetu ina amani ya kutosha na jeshi la polisi
limejipanga vyema kabisa kuwalinda wananchi wote bila ubaguzi wowote
na wajitokeze kwa wingi wakapige kura.
Alisema kuwa nchi ya Tanzania ina utaratibu mzuri sana katika suala la
wapiga kura kwani kila kitu kimewekwa kwa mpangalio mzuri kuanzia
wasimamizi wa uchaguzi hadi wapiga kura hivyo watanzania wakapige
kura bila hofu yoyote kwani serikali imejipanga.
Kihongosi alisema kuwa kupiga kura ni kwenda kufanya maendeleo ya
miaka mitano ijayo hivyo wasisubiri wengine wakachague viongozi
wanaowataka kisha waanze kulalamika kwamba wamechaguliwa viongozi
ambao hawakwenda kupiga kura wajitokeze kukupigia kura chama cha
mapinduzi kwa miaka mitano mingine.