TUKIO LA KWANZA
TAREHE 20.10.2020 MAJIRA YA 18:30HRS KATIKA KITUO CHA MABASI, KATA YA MAGU, WILAYANI MAGU , JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VINGINE VYA DOLA VILIFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA 3 WAKIWA NA KADI 49 ZA WANANCHI MBALIMBALI ZA KUPIGIA KURA KWENYE UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020. KITENDO HICHO NI KINYUME NA MATAKWA YA SHERIA YA UCHAGUZI KWA MTU KUMILIKI KADI YA MPIGA KURA YA MTU MWINGINE KWA MUJIBU WA KIFUNGU CHA 48 (b) CHA SHERIA YA UCHAGUZI SURA YA 343 YA MWAKA 2018. JESHI LA POLISI MKOA W MWANZA HALITOSITA KUCHUKUA HATUA KALI ZA KISHERIA KWA WATU WOTE WANAOPANGA AU KUANZA KUVUNJA SHERIA ZA NCHI ZIKIWEMO SHERIA YA UCHAGUZI.
WATUHUMIWA HAO NI:-
- SHIJA KIMWAGA @MBUNDA, MIAKA 34, MSUKUMA, KATIBU WA KATA WA CHADEMA, MKAZI WA KIJIJI CHA IGOMBE.
- PETER MALEMI @ BUTAGE, MIAKA 59, MSUKUMA, MGOMBEA UDIWANI CDM KATA YA KABILA MAGU.
- KULWA PATRICE@SAWASAWA, BIASHARA, MIAKA 40, MSUKUMA, MKAZI WA MAGU MJINI.
TUKIO LA PILI
TAREHE 19.10.2020 MAJIRA YA 18:35HRS KATIKA HOSPITALI TEULE YA WILAYA YA SENGEREMA MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA DEOGRATIUS MEDARD, MIAKA 42, MSUKUMA, MKULIMA, MKAZI WA SENGEREMA ALIFARIKI DUNIA GHAFLA KABLA YA KUPATIWA MATIBABU BAADA YA KUDAIWA KULA CHAKULA KINACHODHANIWA KUWA NA SUMU KWENYE HARAKATI ZA KAMPENI ZA MGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CCM BWANA HAMISI TABASAMU MWAGAO KABLA YA KIFO CHAKE MAREHEMU ALILALAMIKA KUUMWA NA TUMBO NA ALIKIMBIZWA HOSPITALI. UCHUNGUZI KWA KUSHIRIKISHA IDARA ZINGINE ZA SERIKALI UNAENDELEA NA MAHOJIANO KWA WATU KADHAA YAMEFANYWA NA YANAENDELEA ILI KUBAINI CHANZO HALISI CHA KIFO CHAKE.
TUKIO LA TATU
TAREHE 20.10.2020 MAJIRA YA 18:30HRS HUKO KIJIJI CHA CHIBASI, KATA YA NYAMANGA, WILAYANI UKEREWE, MTOTO MCHANGA NEEMA FELICIAN AKIWA NA SIKU 9, MKAZI WA CHIBASI ALIKEKETWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI NA KUSABABISHIWA MAUMIVU MAKALI NA MTUHUMIWA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA GETRUDA FAUSTINE, MIAKA 43, MKEREWE, MKULIMA, MPAGANI NA MKAZI WA CHIBASI AMBAYE NI BIBI WA MTOTO. KITENDO ALICHOKIFANYA MTUHUMIWA NI CHA UKATILI ULIOVUKA MIPAKA NA HAKIWEZI KUVULIWA. MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI HARAKA IWEZEKANAVYO.
USALAMA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU.
MPAKA SASA KAMPENI ZINAENDELEA VIZURI HAKUNA MATUKIO MAKUBWA YA KUTISHA YALIYOTOKEA NA JESHI LIMEJIPANGA VIZURI KUHAKIKISHA AMANI NA UTULIVU VINAENDELEA ILI WANACHI WAJIANDAE VIZURI KUPIGA KURA SIKU YA TAREHE 28, OKTOBA 2020 MWAKA HUU BILA HOFU.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA HALITAKUBALI WALA KUVUMILIA MTU AU KIKUNDI CHOCHOTE CHENYE MIPANGO YA KUFANYA VITENDO VYA UVUNJIFU WA AMANI KWENYE MCHAKATO HUU WA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2020.
IMETOLEWA NA;
Muliro JUMANNE MULIRO – ACP
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
22 OKTOBA, 2020
.