Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya akiongea na waandishi wa wa habari mjini Katavi ambapo alisema amerIdhishwa na kasi ya mkandarasi anayejenga vihenge vya kisasa na ghala chini Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kanda ya Katavi. Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya (kushoto) akizungumza na wakandarasi wa kampuni ya M/S Unia Araj Spoo ya Poland wanaojenga vihenge sita vya kisasa na ghal moja NFRA kanda ya Mpanda jana alipotembelea kukagua mradi huo utakaokamilika Novemba 2020.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (kulia) akiongea na watumishi wa NFRA ofisi ya Mpanda jana mara baada ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa vihenge na maghala.Amewataka watumishi hao kujituma na kufanya kazi kwa weledi ili nafaka iliyohifadhiwa kwenye maghala idumu kwa muda mrefu na kuendelea kuwa bora.
Katibu Mkuu Kilimo Bw. Gerald Kusaya akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji mkoa wa Katavi jana alipowatembelea kukagua utendaji kazi wao changamoto wanazopitia ili kuzitafutia ufumbuzi. Mwonekano wa picha za vihenge vya kisasa vinavyojengwa mjini Mpanda ili kuongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka chini ya NFRA .
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Homera (kushoto) na kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Bw. Abdalla Malela jana wakati wa ziara ya kikazi mkoani Katavi.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya (wa pili toka kulia) akikagua ghala linalojengwa kwenye kituo cha NFRA kanda ya Mpanda. Ghala hilo litakiuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 5,000 za nafaka litakapokamika Novemba 2020.