Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibaha mjini kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM Silvestry Koka akizungumza na kufafanua jambo kwa wananchi wa kata ya Tangini ambao walifika kwa ajili ya kusikiliza sera zake ili kuweza kumpa ridhaa ya kumcgagua tena katika kipindi cha miaka mitano.
………………………………………………………………………………………
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kukuz asekta ya michezo hapa nchini Mgombea ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amesema atahakikisha kwamba anaboresha viwanja vya michezo mashuleni ikiwa sambamba na kuinua na kukuza vipaji mbali mbali hususan vya wanawake kwa ajili ya kuunda timu ya mchezo wa netiboli.
Koka aliyasema hayo wakati wa mkutano wake wa kampeni kwa wananachi wa kata ya Tangini kwa ajili ya kuweza kunadi sera zake pamoja na kuomba kuchaguliwa kwa kishindo katika uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Octoba 28 mwaka huu.
Mgombea huyo alisema kwamba sekta ya michezo ni moja ya fursa kubwa kwa vijana na wanawake katika suala zima la ajira kwa hivyo endap atachaguliwa kuingia madarakani kwa kipindi kingine cha miaka mitano ataweza kushirikiana nawadau mbali mbali wa michezo pamoja na serikali ili kuweza kutimiza malengo ya kukuza michezo.
Aidha aliongeza kwamba anatambua kuna wanawake wengi waliopo katika Jimbo la Kibaha mjini wana uwezo mkubwa katika mchezo wa netiboli hivyo atahakikisha kwamba anawaweka kwa pamoja na kuunda timu ya mchezo huo ambayo itakuwa ikishirikiki katika michuano mbali mbali ambayo inaandaliwa na ligi tofauti ambazo zinafanyika katika maeno ya Tanzania.
“Sekya ya michezo ndugu zangu kwa kweli ni muhimu sana katika nchi yetu kwa hivyo mimi suala la wanawake kujiendeleza zaidi katika kuviendeleza vipaji vyao katika mchezo huu wa netioboli kwa kweli sina pingamizi na mimi nina liunga mkono kwa asilimia mia na pindi tu mkinichagua katika miaka mitano mingine nitalifanyia kazi kwa kuwapatia na vifaa vingine kwa ajili ya kufanyia mazoezi,”alisema Koka.
Katika hatua nyingine pia alifafanua kwamba katika kipindi kilichopita mbali na kuwa na mikakati mbali mbali ya kuweza kuleta mabadilio chanya katika sekta ya michezo alishagawa mipira na jezi katika timu mbali mbali za wanaume ambao baadhi ya wachezaji wameweza kunufaika zaidi kutoka na kuanzisha ligi ya mpira ambayo iliweza kuzaa matunda.
Pia alisema kwamba pia lengo lake kubwa ni kuweka mipangp madhubuti kwa kushirikiana na halmashauri ya Kibaha mji katika kutenga maeno ya viwanja mbali mbali ya michezo kwa maeno ya mashuleni na kuvikarabati viwanja vingine ambavyo ni vibovu ili watoto waweze kukuza vipaji walivyonavyo.
Koka aliwahimiza wanawake mbali mabli ambao wana uwezo katika fani ya michezo mbali mbali kujiunga kwa pamoja ili kuwa na urahisi wa kuweza kuwasaidia kwa hali na mali lengo ikiwa ni kupata timu mbali mbali za mpira wa netibori, ,mpira wa miguu, pamoja na michezo mingine amabyo itakuwa na manufaa katika jimbo la Kibaha mjini.