Kikosi cha Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC kimewasili salama mapema asubuhi ya leo jijini Mwanza kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa mzunguko wa nane dhidi ya Yanga mchezo utakaopigwa Jumapili ya Oktoba 25 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa.
KMC FC imeondoka jijini Dar es Salaam leo saa 6.00 asubuhi kwa usafiri wa Ndege ya Air Tazania ikiwa na wachezaji 30, Viongozi pamoja na benchi la ufundi likiongozwa na Kocha Habibu Kondo na kuwasili jijini hapa saa 1.30 asubuhi na kwamba kikosi kinaendelea vizuri na hivyo kinafanya maandalizi ikiwemo kuanza mazoezi leo mchana.
Kwa ujumla benchi la ufundi likiongozwa na Kocha msaidizi wa timu hiyo Habibu Kondo ambaye ameungana na kikosi hicho leo hii wanafanya maandaalizi ya kuhakikisha kwamba KMC FC inakwenda kufanya vizuri katika michezo hiyo mitatu ikiwemo huo wa Yanga.
Mbali na maandalizi ya mchezo huo, KMC FC pia inajiandaa kucheza na Timu ya Grambina katika uwanja wa Gwambina Oktoba 30 mwaka huu pamoja na Biashara katika uwanja wa Karume Musoma Mkoani Mara.
Hadi sasa KMC FC imecheza michezo saba na kushinda mitatu,huku ikitoa zare michezo miwili na kufungwa michezo miwili na kwamba imejipanga katika kuhakikisha kuwa inavuna alama zote tisa katika michezo mitatu ya hivi sasa.