Limesema laiti yangekuwepo makubaliano hayo ya Waislamu kumchagua mgombea wa chama fulani Sheikhe Mkuu, Mufti wa Tanzania, Abubakar Mbwana Bin Zubeir angetoa ufafanuzi kwa mujibu wa ibara ya 84 ya katiba ya BAKWATA.
Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hasani Kabeke alikanusha taarifa hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuwa yapo maneno yanasambaa Waislamu wamekubaliana kumchagua mgombea wa chama kimoja si ya kweli,yametolewa na mtu asiye kiongozi hivyo Watanzania wake makini na weledi wa kuchagua.
“BAKWATA ni chombo pekee kinachowaongoza waislamu chenye kauli ya mwisho katika kutetea na kulinda maslahi yao kwa mujibu wa katiba ya Baraza hilo, hivyo Waislamu wasikubali kurubuniwa na siku ya kupiga kura wamchague kiongozi mwadilifu na mwaminifu atakayelinda amani ya nchi hii.
“BAKWATA haiwaelekezi waumini wake kuchagua kiongozi wa chama chochote isipokuwa wachague kwa umakini kiongozi atakayeendeleza amani na utulivu, ndiyo tunu na kila kitu, atakayendeleza yliyo ya uislamu na imani za dini zingine, amani ikivurugika hawatapata hata fursa ya kufanya ibada na swala za aljamaa,”alisema Sheikhe Kabeke.
Alisema malengo ya baraza hilo ni kuona Tanzania inabaki kuwa kisiwa cha amani na kudumu kwenye amani, hivyo siku ya Oktoba 28 wachague kiongozi si kwa misingi ya imani au kabeba agenda za waislamu kwani hakuna aliyebeba agend yao bali watazame uadilifu na historia ya mgombea.
Sheikhe huyo wa Mkoa wa Mwanza alisema wapiga kuwa wawapime wagombea kwa kuhudhuria mikutano ya kampeni inayoendelea ili kusikiliza sera ili siku ya uchaguzi watimize haki yao kwamba wawatizame kwa tafakuri ya kina wanatoa toa kauli kuwa watashinda uchaguzi si kauli thabiti.
“Hatuwaelekezi kuchagua lakini wapo wenye tuhuma nzito za kushabikia ulawiti na ndoa za jinsi moja, hatuwezi kufumbia macho kwani adhabu ya wanaofanya matendo hayo ni kubwa na niwatoe hofu waislamu waendelee kuwa watulivu na kudumisha amani ya nchi yetu,”alisema.
Aidha Sheikhe Kabeke kuelekea kukamilisha mchakato wa uchaguzi Watanzania watasikia na kuona mengi, hivyo Oktoba 28 wakachague kwa uangalifu na umakini mkubwa an wasifanye makosa yatakayowagharimu kwa miaka mitano huku akiikumbusha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wajibu wa kusimamia haki ili mshindi apatikane kwa haki.
“Sina hofu na NEC kusimamia haki bali kama viongozi wa dini kazi yetu ni kuwakumbusha wajibu wao wasimamie sheria, kanuni, taratibu na katiba pamoja na maadili waliyosaini ili haki itendeke, hatumzuii mtu kuwa na mapenzi na chama chochoe, tunazuia uongo kama huyo aliyewasemea Waislamu uongo kuwa watampigia kura mgombea fulani,”alisema sheikh huyo wa mkoa wa Mwanza.