akiongelea kuhusu lengo la Mradi katika Skimu ya Kilimo cha Umwagiliaji
ya Isinyela, Iliyopo Chimala Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya.
Katika picha ni sehemu ya Miundombu ya asili ya Umwagilaiji inayotumika
na wakulima katika skimu ya Isenyela Wilayani Mbarali. Mradi wa Regrow
unategemea kufanya maboresho ya miundombinu hiyo
Mkulima wa zao la Mpunga Bw. Rahim Mbule, akiongelea kuhusu faida zaidi
anazotegemea kupata baada ya maboresho ya miundombinu ya uwagiliaji.
Na MwandishiWetu;
Mbarali
Wakulima katika
Wilaya ya Mbarali katika skimu ya kilimo cha umwagiliaji ya Makangalawe na Isenyela
wamepatiwa elimu kuhusu Uimarishaji wa chama cha wamwagiliaji juu ya usimamizi na
ufuatiliaji wa matumizi ya maji ya umwagiliaji kupitia mradi wa Regrow
unaolenga kukuza utalii kusini mwa Tanzania na kukuza shughuli mbadala za kiuchumi
zitakazoleta matokeo katika utunzaji wa maliasili na rasilimali maji.
Akizungumza katika
mafunzo hayo mratibu wakiufundi wa mradi huo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
Mhandisi, John Chacha Nyamhanga alisema kuwa,wakulima hao
wanatakiwa kuelewa namna sahihi ya matumizi ya maji katika kilimo hicho ili kusiwepo
na upotevu na upungufu wa maji katika mto Ruaha Mkuu unaotegemewa zaidi na hifadhi
za Taifa za Ruaha na Mwalimu Nyerere usimamizi bora wa rasilimali maji utapelekea
pia upatikanaji maji na uhifadhi wa mazingira ikiwa ni pamoja na vyanzo vya maji.
Sambamba na hilo
Mhandisi Nyamhanga aliongeza kwa kusemakuwa, lengo kuu la mradi nikuwawezesha wakulima
kulinda vyanzo vya maji na kuboresha miundombinu ya umwagiliaji ili kuweza kuongeza
tija naongezeko la maji katika mto Ruaha mkuu kwa ajili ya matumizi ya wanyamapori
ili kuweza kukuza utalii katika ukanda wa kusini na shughuli mbadala za wanchi.
“Mradi Umejikita
zaidi katika kuboresha Miundombinu ya umwagiliaji kwa maana yakuboresha mabanio
ili kuwezesha usimamizi wa maji na kuhakikisha
kwamba wakati wa kiangazi kuna upatikanaji
wa maji ndani ya mito yote ambayo ipo juu ya ardhi OevuyaIhefu inayokusanya maji
kwa ajili ya mto Ruaha Mkuu. Alisisitiza.
Kwa Upande
wake Mhandisi wa Umwagiliaji wa Wilaya ya Mbarali Bw.Karoli Lihala, alisema kupitia
mradi huo Miundombinu ya Umwagiliaji itaboreshwa katika maana ya kusakafiwa pamoja
na mifereji mingine ya kugawa na maji ndani ya skimu
Awali,akiongea
katika Mafunzo hayo mkulima katika skimu ya umwagiliaji ya Isenyela Bw. Rahim
Mbule, alisema ana mategemeo ya kupata mafanikio zaidi kupitia kilimo cha
umwagiliaji baada ya maboresho ya miondombinu.
Mradi huo wa
Regrow unaotekelezwa na Serikaliya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia Wizara
ya Maliasili na utalii, unalenga kuongeza utalii kusini mwa Tanzania katika hifadhi
za taifa za Ruaha, Udzungwa, Mikumi na Mwalimu Nyerere.