*****************************************
Inatuma salamu za Rambi Rambi kwa Familia ya Mhe Salim A Salim- kwa kupoteza nguzo muhimu kwenye familia Mke wake- Mama Amne Salim (Mwenyezi Mungu ailaze Roho yake Mahala Pema Peponi Amin)
Mhe Salim A Salim; ni Kiongozi Mahiri Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania- ndiye Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania China Friendship Promotion Association (TCFPA)
Taasisi ya Tanzania China Friendship Promotion Association TCFPA Iliwakilishwa na Katibu wa Taasisi Ndugu Kahama alifika msibani Sambamba na Mjumbe wa Bodi TCFPA- Bi. Victoria Mwanziva
Katibu; Ndugu Joseph K. Kahama- alisaini Kitabu cha Rambi Rambi kwa niaba ya Mhe. Mizengo Peter Pinda, Makamu Mwenyekiti wa Asasi na Bodi ya Asasi ya Tanzania China Friendship Promotion Association TCFPA
Ubalozi wa China Nchini Tanzania- ulishiriki kikamilifu kufariji familia ya Kiongozi huyu; ambaye amepokea Medali ya Kitaifa ya Urafiki (ambayo ni medali ya Heshima ya juu zaid alizawadiwa kutoka kwa Rais wa China)
Ubalozi wa China uliwakilishwa na Balozi wa China nchini Tanzania Mhe Wang Ke, katika Kusaini Kitabu cha Rambirambi- na salamu za faraja kwa Familia nzima.
Familia ilipokea ujumbe huo na kushukuru kwa faraja katika kipindi hichi kigumu-
Taasisi inaendelea kutoa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa na Umma wa Tanzania kwa msiba huu.