VICTOR MASANGU,PWANI
Mgombea ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) amesema kwamba endapo atachaguliwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu atahakikisha anatatua kero ya ukosefu wa huduma ya maji safi na salama kwa wananachi wa kata ya Viziwaziwa na kata ya Mbwawa pamoja na kuanzisha ujenzi wa shule ya msingi katika mtaa wa Sagare Magengeni na ujenzi wa nyumba za walimu kata ya Mbwawa.
Koka aliyasema hayo wakati akizungumza katika mikutano yake ya kufanya kampeni kwa wananchi wa kata mbili za Viziwa ziwa pamoja na wananchi wa kata ya Mbwawa kwa ajili ya kuweza kujinadi na kuomba kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 28 mwaka huu na kuahidi kuleta maendeleo katika Nyanja tofauti na kutatua changamoto zinazowakabili wananachi.
Alifafanua kwamba anatambua kuna baadhi ya maeneo yaliyopo katika kata ya viziwaziwa hawana huduma ya maji hivyo atahakikisha kwamba anaendelea kuongeza jitihada zaidi kwa kushirikiana bega kwa began a serikali katika kuwaondolea adha ya ukosefu wa maji wananchi hao ambao wamekuwa wakipata shida ya kutembea umbari mrefu.
“Ndugu zangu wananchi wa mtaa wa Sagare katika kata hii ya Viziwaziwa natambua kuna changamoto ya upatikanaji wa maji katika baadhi ya maeneo lakini mimi endapo mtanichagua na kunipa kura nyingi katika uchagzui huu ambao unatarajiwa kufanyika siku ya tarhe 28mwezi huu nitapambana vilivyo ili tumewe kumalizie mikakati ya kusambaza maji katika kila nyumba kwa maana nilishapambana na baadhi ya maeneo wameshaaza kupata huduma ya maji kwa hivyo kikubwa ni kunichagua kwa kishindo,”alisema Mgombea huyo.
Kadhalika alisema kwamba pamoja na kupambana na katika huduma ya maji pia ameahidi kulivalia njuga ssuala la kuanzisha mradi wa ujenzi wa shule ya msingi kwa lengo la kuweza kuwaondolea adha kubwa watoto wadogo kutembea umbari mrefu kwenda katika maeneo mengine na kwamba suala hilo anashukuru kwa kuwa serikali ya mtaa imeshapata eneo kwa ajili ya ujenzi huo.
Koka pia aliwaeleza wananchi wa kata hiyo ya Viziwaziwa kuweka mipango madhubuti katika suala zima la upatikanaji wa huduma ya afya ikiwemo sambamba na ukarabati wa miundombinu ya barabara za mitaa ili ziweze kupitika kwa urahisi katika kipindi chote hasa katika nyakati ya mvua zinaponyesha wananchi wasipate shida ya kuvuka katika baadhi ya maeneo.
Katika hatua nyingine Mgombea huyo wa Jimbo la Kibaha mjini akiwa katika mkutano wake wa kampeni kwa wananchi wa kata ya Mbwawa aliwaeleza nia yake na dhamira katika kuwaondolea changamoto mbali mbali zinazowakabili iliwemo ukosefu wa nishati ya umeme, huduma ya upatikanaji wa maji pamoja na ukosefu wa usafiri wa uhakika.
“Ndugu zangu wananchi wa kata hii ya Mbwawa nataka kuwahakikishia kwamba mimi kama mgombea wenu wa jimbo hilo la kibaha mjini nipo pamoja na nyinyi katika suala zima la kuleta maendeleoa na mbwawa ya wakati ule sio ya sasa kwani kila kukicha chachu ya maendeleo inaonekana hivyo pindi mtakaponichaguza tena yale mambo yote mazuri ambayo tumeshaanza kuyatelekeza ni lazima tusimame imara katika kuyaendelea kwa nguvu moja,”alisema Koka.
Kwa upande wake mgombea kiti cha Udiwani katika kata ya Mbwawa Judith Mruge alisema kwamba kiti kikubwa kilichomsukuma kuwania katika nafasi hiyo ni kushirikiana na wananchi pamoja na serikali kwa lengo la kuibua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo kusikiliza kero zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
Naye Mgombea Ubunge kupitia viti maalumu Mkoa wa Pwani kwa tiketi ya CCM Hawa mchafu alisema kwamba wananchi ni lazima wahakikishe wanaunga mkono juhudi ambazo zimefanywa na Rais wa awamu ya tano Dk.John Pombe Magufuli na kuhakisha kwamba wanachagua viongozi ambao ni wazalendo na nchi yao ili kuweza kuwaletea maendeleo na kuachana na wengine ambao wanaweza kuleta uvunjifu wa amani.