***********************************
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema Jeshi hilo limefanya msako mkali wa kuwakamata wahalifu waliokuwa waitekeleza matukio hayo katika ukanda wa kisiwa cha Pemba pamoja na maeneo mengine huku akieleza kuwa wapo baadhi ya wahalifu waliokimbilia nchi jirani.
IGP Sirro amesema hayo leo wakati alipofanya ziara ya ukaguzi kisiwani Pemba na kuongea na baadhi ya wananchi wa kisiwani humo na kuwataka kuzingatia umuhimu wa amani hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ikiwa pamoja na kuacha kujihusisha na matukio ya uhalifu.