Timu ya Mbeya City imemfuta kazi kocha wake Mkuu Amri Said kutokana na mwenendo wa Timu hiyo kushindwa kufanya vizuri msimu huu.
Kwa sasa timu itakuwa chini ya Kocha msaidizi Mathias Wandiba ambaye ataendelea kuwa msimamizi wa timu hiyo iayoshiriki Ligi Kuu Bara.
Mchezo wake wa mwisho ilikuwa jana Oktoba kukaa kwenye benchi na timu ya Mbeya City ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC.
Kwa msimu wa 2020/21, Mbeya City imejenga ufalme wake nafasi ya 18 kwa kuwa imedumu kwa muda wa raundi saba mfululizo.
Ikiwa imecheza jumla ya mechi saba kibindoni ina pointi mbili kwa kuwa ilipata sare mechi mbili ndani ya ligi na kupoteza jumla ya mechi tano.
Safu yake ya ushambuliaji iliweza kufunga bao la kwanza jana Oktoba 20 wakati ikipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Mwadui FC.