***************************************
Mapema leo Waziri Mkuu Mstaafu John Malecela akiwa nyumbani kwake Jijini Dodoma amejitokeza kuuasa Umma wa Kitanzania kutokana na kauli zilizotolewa na Sheikh Issa Ponda Jijini Dodoma mwishini mwa wiki iliyopita katika majukwaa ya kisiasa wakati wa kumnadi Mgombea wa Urais wa Chama cha Chadema Tundu Lisu.
Moja ya kauli za Sheikh Ponda katika kipidi hiki cha kampeni ni kuwa waumini wa dini ya kiislam wamekubaliana nchi nzima kumchagua mgombea wa chadema ili hali kauli hiyo inaonyesha uchochezi wa kidini nchini na badala yake amewataka kuhubiri amani, utulivu na Usalama hasa kipidi hiki cha kampeni za urais, ubunge na udiwani.
Aidha mheshimiwa waziri mkuu mstaafu john malecela baada ya kusikia kauli hiyo kutoka kwa Sheikh Ponda amesema nchi hii mwalim Nyerere ameiacha katika misingi ya umoja na amani licha ya kuchukia Uchochezi na ubaguzi kwa misingi ya udini na ukabila ametumia fursa hii kukemea na kuonya juu ya kuendekeza hali hiyo jambo ambalo litapelekea mpasuko katika makundi ya Jamii na wakati mwingine kupelekea machafuko.
Mheshimiwa Waziri Mkuu malecela ametoa rai kwa wananchi wa Tanzania kupuuza kauli hiyo kwa hakuna watu wanaoweza kuwalazimisha Kumchagua mgombea kwa msingi wa Dini yake bali waangalie vigezo ambavyo wanavipenda ikiwemo maendeleo na umojawa Kitaifa na kuacha kuendelea kujadili vitu visivyokuwa na manufaa nchini na mwisho aliwataka wanachi wote wa Tanzania kuwa watulivu katika wakati huu ambapo mchakato wa uchaguzi unachukua nafasi yake.