Katibu Mstaafu wa SUKI na Mbunge Mteule wa Jimbo la Bumbuli Mkoani Tanga January Makamba amesema kuwa tunapokwenda kwenye uchaguzi wa kuamua hatima ya nchi ni lazima kuangalia mambo manne ikiwemo ubora wa sera na ilani ,ubora wa Chama pamoja na ubora wa wagombea
Hayo aliyasema wakati wa Mkutano wa Kampeni wa Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi CCM DK John Magufuli uliofanyika mjini korogwe Mkoani hapa ambapo alisema jambo lingine la kuangalia ni rekodi na historia ya vyama katika kutekeleza ahadi zake nakuongeza kuwa historia ya CCM ni kuaminiwa katika uongozi wa nchi na kuongoza nchi hii kwa utulivu na usalama pamoja na ustawi kwa miaka yote.
Makamba ambaye ni Katibu Mstaafu wa SUKI alisem kuwa katika vyama vyote vilivyosajiliwa hakuna hata Chama kimoja chenye sifa na sura ya kitaifa kama Chama Cha Mapinduzi hivyo kwenye uchaguzi huu amewataka wananchi waangalie ubora wa vyama na ubora wa wagombea.
Makamba ambaye anasubiri kuapishwa baada ya kupita bila kupingwa alisema kuwa ubora wa sera na ilani ya CCM ukiilinganisha na ilani ya vyama vyote, ilani ya Chama cha Mapinduzi imebeba mahitaji ,matamanio na matumaini ya watanzania nakwamba ata viongozi wao wanapoinadi wanagusa mambo yote yanayowagusa moja kwa moja wananchi.
“Ukimsikia Rais wetu John Magufuli anavyohutubia kwenye mikutano yake ya kampeni wala hatukani mtu, hamsemi mtu wala hamlalamikii mtu bali anazungumza mambo yanayogusa mahitaji ya wananchi na hiyo ni sifa nyingine aliyonayo Mgombea wetu wa Chama chetu “Alisema Makamba
Alieleza kwamba hakuna Chama kingine katika uchaguzi huu ambacho kinarekodi ya uongozi wa nchi au rekodi ya kutekeleza mambo yaliyoleta ustawi kwa watanzania hivyo wananchi wametakiwa katika uchaguzi huu wasiwe na mjadala wa ubora na historia ya Chama kwani CCM ipo mbali zaidi ukiilinganisha na vyama vingine.
” wagombea wetu waliochaguliwa na CCM kupeperusha bendera ya chama ngazi zote wamechujwa haswa na hata Dk Magufuli amepimwa ,kachujwa na ameonekana anastahili kupewa dhamana ya kuongoza nchi yetu hivyo ifikapo October 28 twendeni tukamchague kwa kura nyingi “Alieleza Makamba ambaye kwasasa anasubiri kuapishwa baada ya kupita bila kupingwa.
Alisisistiza kuwa wakimchagua Rais Magufuli tena ili aongoze miaka mitano ijayo anaimani yale mambo ambayo hayajakamilika yatakamilika na yale ambayo wanayahitaji na hayajaanza yataanza.
Hata hivyo alisema kuna mambo makubwa yamefanyika chini ya uongozi wa Magufuli nakwamba chama Cha Mapinduzi kimesimamia Serikali na Sasa zaidi ya zahanati 20 zinajengwa kwa mpigo katika Jimbo la Bumbuli .