Kocha wa timu ya bodaboda Karagwe, Mwl. Shaban Bakari (kulia) akitoa shukrani kwa Waziri wa Viwanda na Biashara na Mgombea Ubunge jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa(kulia) baada ya kumkabidhi kombe kama ishara ya pongezi kwa kazi kubwa ya kuleta mendeleo katika wilaya ya Karagwe na ishara ya ushindi katika uchaguzi utaofanyika Oktoba 28, 2020 kutokana na ushirikiano na kuunga mkono michezo kwa vijana hasa mpira wa miguu kwa kipindi chote cha miaka mitano, katikati ni mlezi wa timu ya bodaboda Karagwe, kareem Amri. Ihanda, Karagwe 19 Oktoba 2020 (picha na Eliud Rwechungura) Waziri wa Viwanda na Biashara na Mgombea Ubunge jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa akiongea na vijana wa bodaboda na kuwapongeza kwa ushindi wa kombe ligi ya bodaboda ya JPM Bodaboda cup Kagera 2020 ambao walipata kwa kuifunga timu ya bodaboda Miembeni Bukoba mabao matano kwa moja katika fainali ilifanyika katika uwanja wa Kaitaba Bukoba siku ya jumapili. Ihanda, Karagwe 19 Oktoba 2020Vijana wa bodadoda Karagwe wakishangilia ushindi wa kombe la ligi ya JPM Bodaboda cup Kagera 2020 kabla ya kumkabidhi Waziri wa Viwanda na Biashara na Mgombea Ubunge jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa kombe kama ishara ya pongezi kwa kazi kubwa ya kuleta mendeleo katika wilaya ya Karagwe na ishara ya ushindi katika uchaguzi utaofanyika Oktoba 28, 2020 kutokana na ushirikiano na kuunga mkono michezo kwa vijana hasa mpira wa miguu kwa kipindi chote cha miaka mitano. Ihanda, Karagwe 19 Oktoba 2020kombe la ligi ya JPM Bodaboda cup Kagera 2020 likiwa tayali mikononi mwa timu ya Bodaboda ya Karagwe baada ya kuibuka mshindi katika fainali dhidi ya timu ya Bodaboda ya Miembeni Bukoba kwa mabao 5 kwa moja iliyochezwa katika uwanja wa kaitaba bukoba siku ya jumapili. Ihanda, Karagwe 19 Oktoba 2020.
*************************************
Na Eliud Rwechungura
Ikiwa ni siku moja baada ya timu ya bodaboda wilaya ya Karagwe kuibuka washindi wa kombe la ligi ya bodaboda ya mkoa wa kagera iliyojulikana kama “JPM BODABODA CUP KAGERA 2020”, Vijana hao wa bodaboda wameamua kumkabidhi kombe hilo Waziri wa Viwanda na Biashara na Mgombea Ubunge jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa kama ishara ya pongezi kwa kazi kubwa ya kuleta mendeleo katika wilaya ya Karagwe na ishara ya ushindi katika uchaguzi utaofanyika Oktoba 28, 2020.
Vijana wa bodaboda Karagwe wamefikia maamuzi hayo ikiwa ni ishara ya shukrani kwa Bashungwa kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa kipindi cha miaka mitano kwa mambo makubwa mawili kwa vijana ikiwa ni kuwa mtetezi mkubwa wa bodaboda na kuwaondolea tatizo kubwa la kusumbuliwa barabarani na matatizo mbalimbali waliyokuwa wanakumbana nayo pia kutambua sekta ya michezo kwa uwepo ligi ya Bashungwa Karagwe Cup kila mwaka ambayo huinua vipaji vya vijana katika wilaya ya Karagwe.
Nae, Waziri wa Viwanda na Biashara na Mgombea Ubunge jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa baada ya kukabidhiwa kombe hiyo amewapongeza vijana wa bodoboda kwa ushindi wa kombe ligi ya bodaboda kimkoa walilolipata ambao unaendelea kuiweka wilaya karagwe katika nafasi nzuri ya kimichezo katika mkoa kagera na Tanzania kwa ujumla, pia akatumia nafasi hiyo kumpongeza mkuu wa mkoa kagera,Brig. Gen. Marco Gaguti kwa kuandaa ligi hiyo ambayo pia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuinua michezo kwa vijana.
Bashungwa ametumia nafasi hiyo kwa kugusa hisia na haja ya vijana wa karagwe kwa kuahidi kutatua changamoto kubwa ya ukosefu wa uwanja wa uhakika, ambapo amewahakikishia vijana hao, kama atachanguliwa na wanakaragwe oktoba 28 kurudi bungeni, amepanga kumalizia uwanja wa mpira kwa kuuboresha kwa viwango vinavyotakiwa maana aliufanyia matengenezo ya awali mwaka huu kwa kuusawazisha pia amehaidi mwanzoni mwa mwaka kesho kuwepo kwa ligi ya Bashungwa Karagwe cup ambayo kwa kipindi hiki itaanza kwa ngazi ya vijiji.
Aidha, Bashungwa ameipongeza Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuendelea kutambua, kudhamini na kuweka jitiada za kuboresha michezo nchini ambayo imeonekana dhairi baada ya Dkt. John Pombe Mgufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuamua kuamisha taasisi ya kutetea masilai ya michezo na Sanaa ya COSOTA kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara na Kuipereka Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, sambamba na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya 2020 – 2025 ambayo pia inaeleza mipango ya kuinua michezo Sanaa na utamaduni kwa vijana.
Kwa upande wake Kocha wa timu ya Bodaboda Karagwe na Mwakilishi wa bodaboda, Mwl. Shaban Bakari ametoa shukrani za kipekee kwa Waziri wa Viwanda na Biashara na Mgombea Ubunge jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa ushirikiano na kuunga mkono michezo hasa mpira wa miguu kwa kipindi chote cha miaka mitano ambapo amekuwa mdhamini mkuu wa timu nyingi ndani ya wilaya ya karagwe pia akatumia muda huo kueleza lengo la kumkabidhi kombe hilo ambayo ni ishara ya pongezi kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa mika mitano na ishara ya ushindi atakaopata katika uchanguzi utakaofanyika Oktoba 28 wa kuendelea kuwakilisha jimbo la Karagwe katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka 2020 – 2025.