Muonekano wa hatua za ujenzi wa Daraja Jipya la Wami litakalokuwa na urefu wa mita 510 na upana wa mita 11.85 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa kilomita 3.8 ukiendelea mkoani Pwani.
Kazi za ujenzi wa nguzo za Daraja Jipya la Wami zikiendelea mkoani Pwani. Hadi sasa ujenzi wa daraja hilo umefikia asilimia 45, unagharimu kiasi cha shilingi takribani bilioni 67.8 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Septemba 2021.
Taswira ya Daraja la Sasa la Wami linalotumika lenye urefu wa mita 88.75, lililopo mkoani Pwani. Daraja hili ni kiungo muhimu kati ya Chalinze na mikoa ya Kaskazini nan chi jirani.