Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge,akizungumza kwenye Semina ya wastaafu iliyoandaliwa na benki ya CRDB kwa lengo la kuwajengea uwezo kwa kutunza na kuwekeza katika masuala mbalimbali yanayopatikana katika benki hiyo leo jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakisikiliza hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (hayupo pichani) wakati wa Semina ya wastaafu iliyoandaliwa na benki ya CRDB kwa lengo la kuwajengea uwezo kwa kutunza na kuwekeza katika masuala mbalimbali yanayopatikana katika benki hiyo leo jijini Dodoma.
Meneja wa Benki ya CRDB Kada ya Kati Bi.Chabu Mishwaro,akitoa taarifa jinsi walivyobunifu wazo hilo kwa wastaafu katika semina ya wastaafu iliyoandaliwa na benki hiyo yenye lengo la kuwajengea uwezo kwa kutunza na kuwekeza katika masuala mbalimbali yanayopatikana katika benki hiyo leo jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Semina ya wastaafu iliyoandaliwa na benki ya CRDB kwa lengo la kuwajengea uwezo kwa kutunza na kuwekeza katika masuala mbalimbali yanayopatikana katika benki hiyo leo jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amesema adhma ya serikali ni kuhakikisha inatengeneza maisha bora kwa wastaafu wote nchini kwa kuwajengea mazingira endelevu ya kujiingizia kipato
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dodoma wakati wa mafunzo maalumu yaliyoandaliwa na benki ya CRDB kwa wastaafu hao yenye lengo ya kutoa fursa zinazopatikana hivyo serikali imeaandaa mikakati kwa kushirikiana na benki hiyo ili kutoa fursa zitakazo wawezesha wastaafu nchini kuanzisha miradi yenye tija .
”Naipongoeza CRDB kwa kuendelea kuwa wabunifu kwa kuja na wazo hili la kuwakutanisha wastaafu ili kujadili kwa pamoja fursa zinazopatikana katika benki hii ukizingatia kundi hili la wateja limekuwa likisahaulika”amesema Dkt.Mahenge
Aidha amesema kuwa CRDB imefanya jambo kubwa kwa kufanya semina kwa wastaafu maana ni kitu kigeni kwa benki ya mikopo kuwakutanisha wastaafu kwa kujadili pamoja na kuwapa mbinu na ujuzi kwa kunijiendeleza kimaendeleo kwa kuongeza kipato.
Dkt.Mahenge amewapongeza wastaafu wote walioitikia wito kwa kuja kujifunza mafunzo masula ya kibenki zitolewazo na CRDB imani yangu baada ya kongamano hili kutakuwa na mabadiliko makubwa katika utunzaji na uwekaji wa fedha pamoja na masuala ya mikopo.
”Leo ni siku muhimu kwa CRDB kwa kutukusanya hapa hivyo naamini baada ya mafunzo hayo tutapata elimu jinsi ya kuwekeza na kutunza masuala ya mikopo katika kuboresha maisha yetu”amesema Dkt.Mahenge
Hivyo niipongeza CRDB kwa kuanzisha na kutekeleza mpango huu wa uwezeshaji kwa wastaafu wenye lengo la kuleta faraja na kuwasaidia wastaafu katika kukidhi mahitaji yao mbalimbali ya kimaisha zote tumekuwa tukiona changamoto hivyo mpango huu utaleta tumaini jipya.
Kwa upande wake Meneja wa Benki ya CRDB Kada ya Kati Bi.Chabu Mishwaro,amesema kuwa CRDB ni bunifu ni benki ambayo inasikiliza mahitaji yote ya Mtanzania kwenye familia yake tunajua tunatengemeana sana katika kusikilizana masuala mazima na mahitaji kwa wateja wetu.
”Hivyo benki yetu tumeamua kubuni ubunifu kwa wastaafu kwa kuwaleta hapa leo na kuwafunza namna ya kuwajengea uwezo pamoja fursa mbalimbali zilizopo katika benki yetu na jinsi ya kutumia mikopo pindi wanavyostaafu wajione kama bado wapo kazini”amesema Bi.Mishwaro