Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Kheri James akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Omary Lumato walipokuwa Jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Kiranyi iliopo ndani ya halmashauri ya Arusha DC mkoani Arusha (picha na Woinde Shizza ,ARUSHA)
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Kheri James(MCC)akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni za kumnadi Mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Magharibi Noah Saputu katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Kiranyi iliopo ndani ya halmashauri ya Arusha DC mkoani Arusha
Mwenyewe wa UVCCM mkoa Arusha Omary Lumato Akiongea akimuombea kura Rais Magufuli katika mkutano wa adhara uliofanyika katika kata ya Kiranyi
wananchi wa Kijiji Cha Kiranyi wakiwa wamenyoosha mikono juu ishara ya kumpigia Kura Rais Magufuli
…………………………………………………………………………………………………
Na Woinde Shizza , Arusha
Mwenyekiti wa UVCCM taifa Kheri James amewasii wananchi wa Jimbo la Arumeru magharibi kuichagua CCM kwasababu ndio Chama pekee kilichoahidi katika Ilani yake ita hakikisha inawezesha miradi mikubwa ya kimkakati itakayo zalisha Ajira kwa vijana Na Wakinamama wengi zaidi wa Kitanzania.Aliyasema hayo Jana wakati alipokuwa akimuombea Kura mgombea Urais kwa tiketi ya chama Cha mapinduzi John Magufuli ,mbunge wa Jimbo hilo Noah Lembrus pamoja na mgombea udiwani wa kata ya Kiranyi Lorivi Muro mkutano uliofanyika katika viwanja vya barazani Ngateu ,iliopo ndani ya halmashauri ya Arusha Wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Alibainisha kuwa ni vyema wananchi wasirudie kufanya makosa waliyoyafanya katika uchaguzi iliopita wa mwaka 2015 ambapo walimnyima Rais Kura pamoja na madiwani ,lakini pamoja na yote hayo Rais hakuwatupa bali aliweza kuwaletea Maendeleo ikiwemo Mradi mkubwa wa maji wa zaidi ya bilioni 520 ,umeme ,zahanati pamoja na kuwa kutoa elimu bure kwa watoto wetu.
Alisema kuwa nivyema wakafanya Maamuzi na kuchagua kiongozi ambaye ataweza atawaletea Maendeleo ,atakae jali shida za wananchi ,atakaeweza kushirikiana na wananchi na kupeleka shida zao bungeni ili ziweze kutatuliwa na Serikali na sio kuchagua viongozi ambao wakiwatuma kuwawakilisha hawarudi kujua changamoto zao bali wanasubiri kipindi Cha kampeni ndio wanarudi kupiga kelele
Nae Mgombea ubunge Jimbo la Arumeru Magharibi Noah Saputu ametumia fursa hiyo kuelezea malengo yaliyoainishwa kwenye Ilani ya chama Cha mapinduzi kwa kipindi Cha miaka mitano ijayo Na kuwaahidi kutekeleza yale yote aliyowaahidi mara baada ya kushinda katika jimbo hilo.
Alisema anatambua katika kata ya Kiranyi kuna changamoto kubwa ya ukosefu wa maji pamoja na barabara ,ambapo alifafanua kuwa wakimpa ridhaa ya kuongoza Mambo ambayo ataanza kuyashulikia ni maswala haya ili wananchi wa kata hiyo waachane na kero hii.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Omary Lumato alisema kuwa Kama wanapenda maendeleo, wanahamu ya maendeleo wachague timu ya watu ambao wanaoweza kuwaleta maendeleo mazuri ambayo yataweza kufanya nchi yetu kuwa Kama Ulaya
Aliwataka wananchi wasifanye makosa maana magufuli ajawabagua japo katika kipindi kilichopita walimnyima Kura Ila yeye kwakuwa Ni Rais wa wote amewapa miradi mikubwa ya maji bilioni 520 ambayo kupitia fedha za halmashauri wasingeweza kupata labda ipite miaka 143 ijayo.