VIGOGO, Al Ahly wametanguliza mguu mmoja katika Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Wydad Athletic Club kwenye Nusu Fainali ya kwanza ya michuano hiyo Uwanja wa Mohamed V Jijini Casablanca, Moroccco usiku wa jana.
Mabao ya Al Ahly yamefungwa na Mohamed Magdi Afsha dakika ya nne na Ali Maaloul dakika ya 62 kwa penalti kwenye mchezo huo wa kwanza wa kimataifa wa mashindano barani tangu janga la COVID-19 miezi sita iliyopita.
Kipigo hicho kinavunja rekodi ya Wydad kutofungwa nyumbani kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya mechi 26.
Na ni hao hao Ahly waliokuwa timu ya mwisho kuifunga Wydad kwenye ardhi yao, Julai mwaka 2016.
Kwa ushindi huo, Pitso Mosimane anaendeleza rekodi yake ya kutofungwa tangu aajiriwe Ahly mwezi uliopita.
Sasa Al Ahly itahitaji kuulinda ushindi huo kwenye mchezo wa marudiano Oktoba 23 Jijini Cairo, Misri ili watinge fainali kwa mara ya 13 katika historia yao.

Nusu Fainali nyingine ya Ligi ya Mabingwa inafuatia leo kwa mchezo kati ya Raja Casablanca na Zamalek kuanzia Saa 4:00 usiku hapo hapo Uwanja wa Mohamed V.