Home Siasa MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KIBAHA MJI CCM APANIA KUWAJENGEA WANANCHI WA KONGOWE...

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KIBAHA MJI CCM APANIA KUWAJENGEA WANANCHI WA KONGOWE KITUO CHA AFYA

0

Mgombea ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Sylvestry Koka kupitia tiketi ya Chama cha mapinduzi (CCM) akizungumza katika mkutano wa kampeni uku akiwa ameshika mkononi ilani ya chama hicho akiwaonnyesha  baadhi ya wananchi wa kata ya Kongowe hawapo picha  waliofika kwa ajili ya kumsikiliza sera zake ikiwa ni maandalizi za kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika octoba 28 mwaka huu.

 Mgombea Ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Sylvestry Koka akiwa anawahutubia wananchi wa kata ya kongowe na maeneo mengine ya jirani katika mkutano wake uliondaliwa kwa ajili ya kampeni ili kuweza kujinadi na kuomba kura kwa wananchi hao.

Mgombea ubunge jimbo la Kibaha mjini akiwa anasisitiza jambo kwa wananchi waliohudhulia katika mkutano huo kuhusina na jinsi atakavyopambania ujenzi wa kituo cha polisi sambamba na ujenzi wa kituo cha afya.

Mke wa Mgombea Ubunge wa jimbo Kibaha mjini Slyvestry Koka akiwa jukwani kwa ajili ya kumwombea kura mume wake  aweze kuchaguliwa tena katika kipindi cha miaka mitano katika kuelekea uchaguzi mkuu .

Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi CCM pamoja na baadhi ya wananchi wengine wa kata ya kongowe wakiwa wametulia katika mkutano huo wa kampeni kwa ajili ya kusikiliza sera na mikakati aliyojiwekea mgombea ubunge wa jimbo la kibaha mjini.

**************************************

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

Mgombea Ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Slvestry Koka ameahidi kulivalia njuga suala la changamoto inayowakabili wananachi hususan wakinamama wajawazito kwa kuhakikisha anapambana kwa kushirikiana na serikali ili kujenga kituo cha afya pamoja na ujenzi wa kituo cha polisi ili kuwaondolea adha wananchi ya kutembea umbari mrefu kwenda kufuata huduma.

Koka aliyasema  hayo wakati  akizungumza na wananchi wa kata ya kongowe katika mkutano wake wa kampeni kwa ajili ya kujinadi sera zake pamoja na kuelezea mikakati yake ambayo ataifanya ya kuwaletea wananchi maendeleo endapo i atachaguliwa tena katika kipindi kikingine cha miaka mitano katika uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika octoba 28 mwaka huu.

Alisema kwamba anatambua kuwa kuna changamoto kwa wananachi wa kata ya kongowe juu ya suala la upatikanaji wa huduma ya afya pamoja na kituo cha polisi hivyo atahakikisha kwamba anashirikiana na serikali katika kuanzisha mradi wa ujenzi katika maeneo hayo ili kuweza kuwasaidia wananchi kuondokana na usumbufu ambao wamekuwa wakiupata.

“Naombeni katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu msifanya makosa kitu kikubwa ni kuendelea kuniamini mimi ili niweze kuendelea kutatua changamoto mbali mbali amabzo zinawakabili wananchi na kitu ambacho ninaweza kusema nitakisimamia kwa nguvu zangu zote ni kuanzisha mpango wa ujenzi wa zahanati, kituo cha afya pmoja na ujenzi wa kituo cha polisi,”alisema Koka.

Alifafanua kuwa endapo ujenzi wa kituo cha afya utakapokamilika utakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa kata ya kongowe pamoja na maeneio mengine ya jiraji kuweza kupata huduma ya matibabu kwa ukaribu na kuondokana kabisa na changamoto ya kwenda kufuata huduma hiyo katika maeneo ya mbali.

Pia aliongeza kuwa wananachi wa kata ya kongowe baadhi yao wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa pindi masuala ya uharifu yanapojitokeza hivyo ataweka mipango madhubuti kwa kushirikiana na wananchi kuweza kupata ujenzi wa kituo cha polisi ili kusaidia kutoa huduma ya ulinzi pamoja na mambo mengine ya kiusalama.

Katika hatua nyingine Mgombea huyo alisema kwamba lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba anaweka mikakati mizuri amabyo itaweza kuwasaidia wananchi kuondokana na wimbi la umasikini kwa kuhakikisha kuwa anaviwezesha vikundi mbali mbali vya ujasiriamali ili viweze kufikia malengo ambayo vimejiwekea katika kukuza uchumi wao.

Kwa upande wake Mgombea udiwani wa kata ya Kongowe kupitia tiketi ya CCM  Hamisi Shomari alisema  kwamba endapo atachaguliwa katika uchaguzi mkuu atahakikisha kwamba anashirikiana bega kwa bega Mbunge katika kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi katika  huduma mbali mbali za kijamii ikiwemo suala la huduma ya maji safu na salama pamoja na  elimu.

Naye Mke wa mgombea huyo  Selina Koka  hakusita  kupanda jukwani  na kupiga magoti  kwa ajili ya kumwombea kura mumeo  na kuwahimiza wananchi  wa kata ya kongowe na waweze kumchagua kwa kishindo ili aweze kutatua changamoto zao na  kuwaletea chachu ya  maendeleo.