Katibu wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Dodoma Mjini (UWT), Diana Madukwa,akizungumza na viongozi wa Dini alipokutana nao kuhusu kuwahamasisha waumini kuendelea kutunza Amani wakati tunapoelekea katika Uchaguzi leo jijini Dodoma.
Mchungaji wa kanisa la Tanzania Assembles of Good,Mchungaji Marcel Mushi,akitoa neno la shukrani kwa Katibu wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Dodoma Mjini (UWT), Diana Madukwa (hayupo pichani) alipokutana kuzungumza na viongozi wa Dini kuhusu kuwahamasisha waumini kuendelea kutunza Amani wakati tunapoelekea katika Uchaguzi leo jijini Dodoma.
Katibu wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Dodoma Mjini (UWT), Diana Madukwa,akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Dini mara baada ya kuzungumza nao kuhusu kuwahamasisha waumini kuendelea kutunza Amani wakati tunapoelekea katika Uchaguzi leo jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Kamati Maalum za Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT), Wilaya ya Dodoma,imewaasa viongozi wa Dini,kushawishi waumini wao kutunza amani katika kipindi hiki wakati Taifa likitarajia kufanya uchaguzi wa Rais,wabunge na madiwani watakaoongoza kwa kipindi cha Miaka Mitano ijayo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Katibu wa UWT Wilaya hiyo, Diana Madukwa,alipokutana na Viongozi wa Dini ambapo amesema kuwa bila Amani hakuna jambo litakalofanikiwa bila kuwepo kwa Amani.
“Ndugu zangu viongozi,sisi chama cha Mapinduzi tunaamini ninyi mnaushaishi mkubwa wa kuwasisitiza waumini wenu juu ya kutunza Amani,na kuwachagua viongozi wa chama cha mapinduzi CCM”amesema Madukwa
Aidha amesema kuwa na sisi waumini tunaokuja katika nyumba za Ibada tunaomba muendelee kutusisitiza umuhimu wa Amani ,
”Ninyi mnailea jamii,tukaona ni bora tukutane nanyi na tuwaambie jamii inawategemea ninyi,lakini kubwa la kwanza tunaomba muemdelee kuliombea taifa letu amani, tusije tukapata machafuko katika kipindi hiki cha uchaguzi”amesisitiza Madukwa
Kwa upande wake Mchungaji wa kanisa la Tanzania Assembles of Good,Mchungaji Marcel Mushi amesema kuwa wana matumaini makubwa uchaguzi huu utakuja na viongozi wazalendo.
”Bila shaka tumeshuhudia mabadiliko makubwa ya maendeleo katika serikali hii,na tunamini watakaojitokeza kupiga kura watawachagua viongozi bora”amesema Mchungaji Marcel.