**********************************
NJOMBE
Licha ya Tanzania kuwa mzalishaji mkubwa wa Nyama na Maziwa lakini inaelezwa bado kuna kiwango kidogo zaidi cha matumizi ya vyakula hivyo ambavyo muhimu zaidi katika kujenga afya ya binadamu.
Akitoa takwimu za serikali Katibu Mkuu wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt Rashid Tamatamah amesema katika kipindi cha mwaka 2019/20 Tanzania imezalisha maziwa bil 3 wakati mwaka wa nyuma ikizalisha lita bil 2 hatua ambayo inatajwa kuchangiwa na ongezeko la Ng’ombe pamoja na maboresho makubwa yaliofanywa na serikali katika ya mifugo,uvuvi na kilimo.
Kuhusu zao la Nyama Tamatamah pia amesema kuna ongezeka la uzalishaji kutoka tani laki 6.9 zilizozalishwa mwaka 2018/19 hadi tani laki 7.16 katika mwaka wa serikali 2019/2020 jambo ambalo limekuwa na matokeo chanya katika kukuza uchumi wa nchi huku pia akiwataka wananchi kujenga utamaduni wa kula vyakula bora kwa kuzingatia kanuni za lishe ili kuepukana na changamoto ya udumavu wa akili na maarifa.
“TNchi yetu inazalisha kiwango kikubwa cha maziwa na Nyama lakini cha kushangaza bado watu wanachangamoto ya udumavu hivyo tuanze kujenga utamaduni wa kunywa maziwa na nyama ili kukidhi mahitaji ya mwili kwa mujibu wa shirika la chakula duniani” Alisema Dkt Tamatamah .
Katika hatua nyingine Kaimu Mkurugenzi huduma, wizara ya Mifugo na Uvuvi idara ya Utafiti mafunzo na huduma za ugani Dkt Kejer Gillah amesema Watanzania Wengi wamekuwa na hawali vyakula vyenye protini ya daraja la kwanza kama vile nyama na samaki jambo ambalo limekuwa changamoto katika makuzi ya watoto na afya bora ya akili.
Dkt Gillah anasema njia pekee ya kuepukana na udumavu ni kuzingatia mlo wa makundi yote ya chakula na kudai kwamba ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya njema serikali kupitia wizara ya kulimo na uvuvi imekuwa ikifanya tafiti mbalimbali za vyakula vinavyofaa kwa matumizi ya binadamu.
“Idadi kubwa ya watanzania wanakosa vyakula vyenye protein ya daraja la Kwanza jambo ambalo limekuwa na athari katika afya ya akili na kwamba kupitia maonyesho hayo wizara inatumia fursa hiyo kutoa elimu kwa umma”Alisema Dkt Kejeri Gillah.
Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa Njombe ambao wamejitokeza katika viwanja vya maonyesho Akiwemo Titho Mng’ong’o wanasema wamefurahishwa na kitendo cha serikali kuupa heshima mkoa wa Njombe kuwa mwenjeji wa maonyesho hayo kw kuwa wameweza kupatiwa elimu mbalimbali za lishe pamoja na kupewa ujuzi wa matumizi ya teknolojia mbalimbali za kilimo.
“Tunashukuru kupitia maonyesho haya tumeweza kujifunza mambo mengi ambayo yanafaida kwetu na kwamba tunakwenda kuyafanyia kazi ipasavyo”,Alisema Titho Mng’ong’o