Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba Akisalimiana na Mwakilishi Wa Askofu wa Jimbo la Mbinga Padre Josephat Malunda katika Kongamano la kuliombea Taifa ili liwe na Amani na umoja, kuombea uchaguzi Mkuu, upite kwa amani na utulivu,lilofanyika katika uwanja wa Polisi jana Wilayani Nyasa.Katikati ni Mgombea Ubunge CCM, wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stela Manyanya
………………………………………………………………………………………….
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba, amewataka wananchi wa Wilaya ya Nyasa kutoa Taarifa ya Vitendo vinavyoashiria Uvunjifu wa amani, ikiwemo wahamiaji haramu, wanaoweza kuingia Nchini Tanzania kupitia Mpaka wa Nchi jirani ya Malawi na Msumbiji.
Ameyasema hayo jana wakati akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria katika Kongamano la Kuombea Amani na Utulivu wa Nchi yetu, kuelekea Uchaguzi Mkuu, na Kumuenzi Rais wa Kwanza wa Nchi ya Tanzania, Baba wa Taifa Mwl Julus K. Nyerere lilofanyika katika Uwanja wa Polisi,Mbamba bay, Wilaya ya Nyasa.
Chilumba alifafanua kuwa, anawapongeza sana wananchi wa Wilaya ya Nyasa, kwa Ushirikiano anaopewa na Wananchi wa Wilaya hii hasa, katika kuzuia Vitendo vya kihalifu ikiwa ni pamoja na kutowaruhusu wahamiaji Haramu kuingia Nchini, kutoka Nchi ambazo tunapakana nazo kwa mipaka ya majini yaani Nchi ya Malawi na Kwa Upande wa Nchi kavu ni Nchi ya Msumbiji.
Aliongeza kuwa, Wilaya ya Nyasa imelazimika kuadhimisha, kufanya kongamano hilo kwa malengo ya kuliombea Taifa ili liwe na Amani na umoja, kuombea uchaguzi Mkuu, upite kwa amani na utulivu, kuombea Elimu,na Afya kwa Watanzania, kuwaombea Viongozi wa Dini na Serikali, Uchumi na Maendeleo na Kumwombea, Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere Astarehe kwa amani kwa kuwa ndiye aliyeweka misingi ya Umoja na amani wa Nchi yetu ya Tanzania.
“Napenda kuchukua Fursa hii kuwapongeza wananchi wa wilaya ya Nyasa kwa Ushirikiano wenu mnaonipa wa kuwafichua wahalifu na hatimaye wilaya inakuwa salama.Hivyo ninaomba muendelee kutoa taarifa ili tuweze kupambana na wahalifu lakini kikubwa tuiombee Tanzania iwe na amani hasa kipindi hiki tunachoelekea uchaguzi Mkuu.”
Aidha alimpongeza Rais John Pombe Magufuli kwa uchapakazi wake, pia kuipa Wilaya ya Nyasa miradi mingi Mikubwa ya Maendeleo, ambayo kumeifanya Nyasa kuwa na Fursa za kichumi. Kwa hiyo ili Tuweze kuzitumia fursa hizo ni lazima tuwe na Amani na utulivu ndipo kila mtu ataweza kufanya kazi kwa bidii.
Naye Mgombea Ubunge Kupitia CCM Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya ambaye pia ni Naibu waziri wa Viwanda na Biashara, akiongea kwa niaba ya Viongozi wa Serikali alisema ameipongeza Wilaya ya Nyasa kwa kufanya kongamano hilo la kuiombea amani Nchi yetu ya Tanzania, na hasa kumuombea Hayati Mwl.Julius k. Nyerere, ambaye ndiye Rais wa kwanza wa Tanzania, aliyeweka Msingi wa Amani Umoja na Utulivu Kwa Nchi ya Tanzania.
Hivyo aliwataka wananchi wa Wialaya ya Nyasa, kushirikiana katika kujiletea maendeleo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kushiriki kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, na kukuza pato la kaya ili kulinda falsafa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ya “HAPA KAZI TU” inayowataka wananchi kufanya kazi kwa juhudi na Kujitegemea.
Kongamano hilo limehudhuriwa na waumini wa Dini zote za Kiislamu, na kikristo, Viongozi wa Dini , pamoja na wagombea wote wa nafasi za Udiwani na Ubunge wa Vyama vyote vya Siasa Wilayani Nyasa.
Imeandikwa Na Netho c.Sichali
Afisa habari Nyasa dc.0767417597 au0623714299