UMATI wa Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Micheweni wakifuatilia mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar kwa kupitia CCM Mhe.Dk Hussein Ali Hassan Mwinyi, uliofanyika katika Uwanja wa Micheweni Pemba leo 15/10/2020.
MGOMBEA Uwakilishi kupitia Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Micheweni Ndg.Shamata Shaame Khamis, akizungumza kwa niaba ya Wagombea Uwawakilishi, Ubunge na Udiwani wa CCM wa Wilaya ya Micheweni Pemba, uliofanyika uwanja wa micheweni
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi akizungumza wakati wa mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Zanzibar uliofanyika katika viwanja vya micheweni Wilaya ya Michewni Pemba.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe DK.Ali Mohamed Shein, akihutubia katika mkutano wa kampeni ya CCM ya Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Ali Hassan Mwinyi uliofanyika katika uwanja Skuli ya Micheweni Pemba na kumuombea Kura Mgombea Urais wa Zanzibar na Wagombea wote wa CCM.
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Ali Mohamed Shein, akiwatambulisha Wagombea Ubunge,Uwakilishi na Madiwani wa CCM wa Wilaya Micheweni katika mkutano wa kampeni ya CCM uliofanyika katika uwanja wa Skuli ya Michewni Mkoa wa Kaskazini Pemba
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akifuatlia mkutano wa Kampeni ya ya Uccm ya mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Dk. Hussein Mwinyi na (kulia kwa Mama) Mke wa Mgombea Urais wa Zanzibar Mama Maryam Mwinyi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Bi. Leila Ngozi
MWANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi Kisiwani Pemba kutoka Kijiji cha Kizimbani Ndg.Suleiman Abdall Ali, akimshangilia Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe.Dk. Hussein Mwinyi , akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Skuli ya
Sekondari Micheweni leo 15/10/2020
WANACHAMA wa CCM Wilaya ya Michewwni Pemba wakishangilia katika mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe.Dk. Hussein Mwinyi (hayupo pichani) uliofanyika katika viwanja vya Skuli ya Sekondari Micheweni Pemba leo 15/10/2020
MWANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi akimshangilia Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Mhe. Dk. Hussein Mwinyi wakati akihutubia katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Skuli ya Sekondari Micheweni leo 15/10/2020.
WAGOMBEA wa Nafasi za Ubunge na Uwakilishi wa Wilaya ya Micheweni Pemba wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni ya CCM uliofanyika katika viwanja vya Skuli ya Sekondari Micheweni Pemba
MGOMEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi, akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Skuli ya Sekondari Micheweni Pemba na kuwaomba kura na kumuombea kura Mgombea Urais wa Tanzania Mhe.Dkt. John Magufuli na kuwaombea kura Wabunge, Wawakilishi na
Madiwani wa CCM.,(Picha na Ikulu)