Home Mchanganyiko SERIKALI YASOGEZA UKATAJI WA LESENI KWA SACCOSS NA VYAMA VYA USHIRIKA VYA...

SERIKALI YASOGEZA UKATAJI WA LESENI KWA SACCOSS NA VYAMA VYA USHIRIKA VYA KUWEKA NA KUKOPA HADI APRIL MWAKANI BADALA YA MWISHO WA MWEZI HUU

0

***********************************

Na Ahmed Mahmoud Arusha

Serikali ipo mbioni kuhakikisha inasajili mfumo wa Teknolojia kwa vyama vya ushirika wa kuweka na kukopa Saccos kwa lengo la kuondoa changamoto ikiwemo kuzitambua sanajari na kuvipa leseni.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mkuu wa Chuo Cha Ushirika Moshi Prof .Alfred Sife Kwenye Kongamano la Maadhimisho ya wiki ya ushirika duniani linalofanyika jijini Arusha.
Alisema dunia imekuwa ikibadilika kimfumo kuendana na teknolojia hivyo wana ushirika wanaowajibu wa kujiendeleza kielimu kuendana na mabadiliko ya teknolojia ili kuendeleza sekta hiyo ambayo imekuwa ya tatu baada ya Taasisi za kibenki.
“Ongezeko la Teknolojia itupeleke kujenga mifumo itakayosaidia kuongeza usalama kwenye vyama vya kuweka na kukopa ambapo tunajiandaa kuwa na mfumo mmoja huu utasaidia kuongeza usalama na kuboresha wigo wa taasisi hizo”
Awali Mchumi Mwandamizi wa Benki Kuu BOT Alli Liyau amesema kuwa Vyama vya ushirika vya kuweka na kukopa kwa ujumla wao vimekuwa na mafanikio na kuweza kushika nafasi ya Tatu kwa umoja wao baada ya CRDB na NMB
Alisema mfumo wa usajili wa vyama hivyo utawasaidia kuweka usalama kujua taarifa kwa kuondoa kutembea kufuata huduma na kuacha kuhifadhi fedha majumbani ambapo usajili huo ulikuwa uwe mwisho 30 mwezi huu na imeongezwa hadi April mwakani.
Nae Makam Mwenyekiti wa ushirika wa kuweka na kukopa nchini  Somoe Ngogwe alisema siku ya ushirika ni siku ya kutafakari kwa kina kwa lengo la kuenzi waasisi na.kutambua mchango wa vyama hivyo kuchangia kukuza uchumi.
Alisema  mchango huo umejenga uchumi jumuishi ambao umeifanya sekta hiyo kushika nafasi ya Tatu kwenye utoaji wa huduma za kifedha kuzidi hata mabenki.
Kwa Upande wake Paul Nandrie kutoka Taasisi ya Mentors Action TMA amesifu mfumo huo ambao ni takwa la kisheria na taasisi hiyo imekuwa ikitoa na kuwafungia vyama vya kuweka na kukopa kwa miezi mitatu ya majaribio bure kwa gharama ya 200’000
Amezitaka Taasisi hizo kuwa wabunifu wa kwenda na wakati kwa kujifunza katika  kiwekeza kwenye mifumo kuwa wabunifu  wa kwenda na teknolojia kwani.matokeo watu wengi watafaidi uchumi jumuishi.