Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akimuombe kura Mgombe Ubunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu |
Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Tanga Lupakisyo Kapange akimuombea kura Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu
Umati wa wananchi wakimsikiliza Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga(CCM) Ummy Mwalimu
Sehemu
ya Umati wa Wakazi wa Kata ya Mzingani Jijini Tanga wakimsikiliza kwa
umakini Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu
Sehemu
ya Umati wa Wakazi wa Kata ya Mzingani Jijini Tanga wakimsikiliza kwa
umakini Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu
Sehemu
ya Umati wa Wakazi wa Kata ya Mzingani Jijini Tanga wakimsikiliza kwa
umakini Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu
Msanii Mchina Mweusi akitumbuiza wakati wa mkutano huo
Msanii wa mziki wa Bongofleva Kassim Mganga akitumbuiza wakati wa mkutano huo wa kampeni
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga
(CCM) Ummy Mwalimu ametangaza neema kwa wavuvi kwenye Jiji la Tanga baada ya
kuwahaidi kwamba watawezeshwa kupata mikopo nafuu na zana za kisasa za uvuvi
ili waweze kunufaika kupitia sekta hiyo na hatimaye kujikwamua kiuchumi.
Sambamba na hilo amehaidi pia
kuipatia ufumbuzi changamoto ya barabara ya kwenda Machinjioni –Msikitini ili
kuhakikisha inakuwa kwenye kiwango kizuri kuliko ilivyokuwa sasa.
Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii Wazee na Watoto aliyasema hayo wakati wa mkutano wake wa
kampeni uliofanyika Dunia Hotel Kata ya Mzingani Jijini Tanga uliohudhuriwa na
umati mkubwa wa wananchi.
Alisema kwamba suala la wavuvi
atalishughukia kwa kuhakikisha changamoto ambazo wanakabiliana nazo wakati wa
utekelezaji wa majukumu yao anazipatia ufumbuzi ili kuwawezesha kufanya
shughuli hizo bila vikwazo.
Ummy alisema pia atahakiksha
anawezesha mazingira ya uwepo wa barabara ya Mzingani hadi Machinjioni kwa
kupasua barabara ya mtaa wa msikitini ili kuwawezesha wananchi kuitumia kwa
ajili ya shughuli zao mbalimbali
“Kuhusu suala la taa za barabara
nitalifanyia kazi kuhakikisha mitaa yote muhimu kwenye kata ya Mzingani inawaka
nyakati za usiku kuweza kulinda usalama wa watoto hivyo ninawaomba wananchi wa
Mzingati mnichague kwani nina mipango mingi ya kimaendeleo lakini pia Octoba 28
mchagueni kwa kuwa nyingi za kishindo Rais Dkt John Magufuli“Alisema
Hata hivyo alisema katika kipindi
cha Miaka mitano iliyopita Serikali ya CCM ilijielekeza katika kujenga
Miundombinu ya Hospitali, Zahanati na Vituo Afya na kuwa katika miaka
mitano ijayo CCM itajielekeza ktk kuhakikisha maboresho ya bima ya Afya ili
watu wengi waweze kupata huduma za Afya bila vikwazo.
Sambamba na hilo Ummy alieleza
kuhusu suala la CT Scan ambapo aliwaambia wana Mzingani kwamba kuna
maneno yanaelezwa kwamba alichukua CT Scan Mashine ya Bombo na kuipeleka
Hospitali ya Mwananyamala DSM.
“Labda niwaambieni wapuuzeni maana
wameanza kupagawa kwanza sisi hatukuwa na hiyo mashine ila kuna mdau alitaka kutusaidia
ikabidi tutafute fedha za kujenga Jengo kwa ajili ya kuiweka mashine hiyo
ambayo itasaidia sana kupunguza safari za kwenda Kilimanjaro na tayari
fedha zimeshapatikana”Amesema Ummy Mwalimu.