MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Dk. Hussein Mwinyi, akiwasalimia wananchi wa Chwaka wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa skuli ya Chwaka Mkoa wa Kusini Unguja.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM, Abdalla Juma Mabodi (kushoto), na mgombea Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, Dk. Hussein Mwinyi, wakiangalia ratiba ya mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa skuli ya Chwaka.
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja, Ramadhan Abdalla Kichupa, akitoa salamu za mkoa huo wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea Urais wa Zanzibar, uliofanyika uwanja wa mpiara skuli ya Chwaka.
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohame Shein, akimkabdhi ilani, mgombea Uwkilishi jimbo la Tunguuu, Simai Mohamed Said katika mkutano wa kampeni uliofnyika Chwaka Mkoa wa Kusini Unguja.
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohame Shein, akimkbidhi ilaniakiwahutubia wananchi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa mpira skuli ya Chwaka hapo jana
WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi CCM, walioshiriki katika mkutano wa kampeni za chama hicho uliofanyika Chwaka Mkoa wa Kusini Unguja jana.
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohame Shein, akimnadi Dk. Hussein Mwinyi (kushoto), kupeperusha bendra ya CCM kwa nafsi ya Urais wa Zanzibar, na Issa Ussi Haji Gavu (kulia) kiwania nafasi ya Uwakilishi jimbo la Chwaka, wakati wa mkutano wa kampeni uliofnyika uwanja wa Chwaka Mkoa wa Kusini Unguja.
PICHA ZOTE NA ABDALLA OMAR)
……………………………………………………………………………………
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk.Hussein Mwinyi amesema endapo atapewa ridhaa ya kuwa rais,ataendeleza miradi yote iliyoasisiwa na serikali ya awamu ya saba na kuanzisha miradi mipya ya kiuchumi.
Alisema serikali ya awamu ya saba imetekeleza Ilani kwa asilimia 90 katika sekta mbalimbali nchini.
Alisema katika Ilani iliyopita wameanza ujenzi wa hospitali ya rufaa ya Binguni katika wilaya hiyo na kwamba yeye atamalizia ujenzi huo.
Alisema katika utawala huo wamepandisha hadhi vituo vya Afya mbalimbali kwa lengo la kuboresha huduma za Afya nchini.
Alisema katika sekta ya elimu Dk.shein,amejenga shule mbalimbali za ghorofa katika Mkoa huo zenye vifaa vya kisasa vya kusomea na kufundishia masomo yote.
Alisema pia zimejengwa barabara mbalimbali za kiwango cha lami katika Mkoa.
Aidha Dk.Hussein,alisema serikali ya awamu ya saba wamefanikiwa kusambaza maji kwa urefu wa kilomita 7.6 kutoka Bambi hadi Uroa.
Akizungumzia vipaumbe vyake alisema kuwa atamalizia miradi yote iliyoanzishwa na serikali ya awamu ya saba ambayo haikumaliza.
Alisema atahakikisha anamaliza migogoro ya ardhi baina ya wananchi na wawekezaji kwa kuweka utaratibu mpya wa kumiliki na kutumia ardhi.
Katika sekta ya maji safi na salama atahakikisha anaendelea kujenga miundombinu ya upatikanaji wa maji.
Aidha kwa upande wa suala la mazingira alisema Kuna baadhi ya wananchi wanatumia mistu kwa ajili ya kujipayia kipato hivyo kwa utawala wake atahakikisha anawapatia kazi mbadala ili kunusuru mazingira yasiharibiwe.
Alisema wajasiriamali wote watapewa mikopo,mafunzo,masoko na mitaji yenye fursa nafuu.
Alisema ameahidi kutoa ajira kwa vijana ukiachilia mbali zile ajira 300,000 zilizotajwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025.
Pamoja na hayo alieleza kuwa patajengwa viwanda vidogovidogo na vikubwa kwa ajili ya kuongeza fursa za ajira.
Alisema kupitia utekelezaji wa mpango wa uchumi wa bahati(blue economy),alisema atahakikisha wavuvi wanapata vifaa vya kisasa vya uvuvi ili kwenda sambamba na mabadiliko ya Mapinduzi ya kiuchumi nchini.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alisema wagombea wote walioteuliwa Wana uwezo na uzoefu wa kukipigania Chama Cha Mapinduzi.
Alisema viongozi hao sio wanagenzi katika medali za kisiasa na kiutendaji kwani kila kiongozi ana uzoefu katika fani yake na majukumu wanayoomba kupewa ridhaa na wananchi.
Alisema viongozi hao watapewa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 ili wakasimamie kwa uadilifu utekelezaji wake kwa kuwatumikia wananchi wote bila ubaguzi.
Alisema Dk.Mwinyi,ndiye aliyepewa dhana ya kupeperusha bendera ya CCM katika kuwania kiti cha urais wa Zanzibar ambaye ni mgombea mwenye uzoefu mkubwa kiutendaji.
Dk.Shein,aliwasihi wananchi wamchague mgombea huyo wa CCM ili aendelee kulinda na kudumisha Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 na Muungano wa Serikali mbili.
Akitaja sifa za mgombea huyo wa kiti Cha Urais wa Zanzibar,Dk.Shein alisema kiongozi huyo amehudumu ndani ya serikali kwa miaka mingi hivyo ana uzoefu mkubwa katika masuala ya uongozi.
Alisema kuwa Dk.Mwinyi, nafasi ya Urais anaiweza na ataongoza nchi kwa mafanikio makubwa kwani amewahi kuhudumu katika Wizara ya Afya,amehudumu katika Wizara ya masuala ya muungano na kushiriki katika vikao na mijadala mbalimbali ya kuimarisha Muungano.
Akizungumzia historia ya Zanzibar toka enzi za ASP kuwa uchaguzi wa pili wa Zanzibar wa January 1961 Chama Cha ASP kilishinda kwa kura nyingi lakini hakikupewa nchi na utawala wa wakati huo.
Alisema kabla ya Mapinduzi wananchi waliishi maisha ya dhiki,tabu na mateso makubwa huku wakikoseshwa haki zao za msingi kwa makusudi.
Makamu Mwenyekiti huyo wa CCM,alieleza kuwa mateso dhidi ya wazawa ndio yaliyochochea harakati za wananchi wa Zanzibar kutafuta njia ya kujikombo kupitia Mapinduzi 1964.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi,alisema CCM imeendelea na kampeni zake chini ya mgombea wake Dk.Mwinyi ambaye anawafuata wananchi wa makundi mbalimbali katika maeneo yake.
Aliwasisitiza mabalozi wa mashina ya CCM kuwa ikifika Octoba 28,mwaka huu wahakikishe wanapita nyumba kwa nyumba kuhamasisha wanachama na wananchi kwenda kukipigia kuwa Chama Cha Mapinduzi.
Alisema Wana CCM wahakikishe wanajitokeza kwenda kutekeleza matakwa ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977,ibara ya tano inayoelekeza kuwa ushindi wa CCM ni lazima kwa kila uchaguzi.
“Wapo baadhi ya viongozi wa kisiasa wameanza kuhamasisha vurugu na ubaguzi wa kikabila na kidini jambo ambalo ni hatari kwa amani ya nchi na ustawi wa maendeleo.
Vijana msikubali kutumiwa na wanasiasa hao wasiokuwa wazalendo Kama wanaka Octoba 27,mwaka huu kufanya vurugu basi waende wao wakapige hiyo kura ya mapema lakini sio kuwahamasisha wananchi wasiokuwa na hatia kuvunja sheria”, alisema Dk.Mabodi na kuiongeza kuwa suala la kura ya mapema lipo kisheria na watu wanaohusika na upigaji wa kura hiyo wanajulikana.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kusini Unguja, Ramadhan Abdallah Ali (Kichupa) alisema ndani ya Mkoa huo CCM ipo vizuri na wanasubiri siku ya kupiga kura ili wakawachague kwa kura nyingi wagombea wote wa chama hicho.
Akizungumza kwa niaba ya wagombea uwakilishi wa wilaya ya Kati ,mgombea uwakilishi wa Jimbo la Chwaka Issa Haji Ussi ,alisema uchaguzi uliopita CCM katika jimbo hilo ilishinda zaidi ya asilimia 80 na mwaka huu wamejipanga kushinda kwa zaidi ya asilimia 90.
Naye mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo Haji Makame Mlenge alisema kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wanashinda katika uchaguzi huo.
Anna Agata Msuya,amesema kuwa Zanzibar imepiga hatua kubwa kimaendeleo chini ya uongozi wa Dk.Ali Mohamed Shein.
Ameeleza kwamba juhudi hizo za maendeleo zitakuwa na manufaa endapo wananchi wa Zanzibar kwa pamoja wataamua kuwachagua wagombea wa CCM kuwa viongozi kuongoza nchi.
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Abdallah Haidar alieleza kuwa CCM imeendelea kufanya siasa za kisitaarabu kwa kufanya kwa kina Sera zake bila kutukana ama kubeza vyama vingine vya kisiasa.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Tabia Maulid Mwita,aliwaomba vijana bila kujali tofauti za kisiasa siku ya kupiga kura wajitokeze kwa wingi kuwapigia kura wagombea wote wa CCM ili nchi iendelee kupaa kiuchumi na kimaendeo.
Naye Mjumbe wa Kamati ya siasa ya CCM ya Mkoa huo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa kusini Unguja Ayoub Mahmoud Mohamed akifafanua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 alisema wamefanikiwa kudumisha amani na utulivu kwa kumaliza mgogoro wa vijiji vya Chwaka na Malumbi.
Pia alisema wamemaliza mgogoro wa vijiji vya Uzi na Ng’ambwa wananchi.
Alisema katika sekta ya kilimo tayari zimetengwa hekta 892 kwa ajili ya kilimo huku wakinunua mashine ya kusindika zao la ndimu kwa lengo la kuongeza thamani zao hilo ili wananchi wanufaike na kilimo.
Ayoub,alisema katika Mkoa huo tayari wamekamilisha ramani ya ujenzi wa daraja la kutoka Unguja ukuu kwenda Uzi.
Pamoja na hayo kwa upande wa sekta ya ufugaji alisema tayari serikali imenunua mashine kwa ajili ya kusindika maziwa ili kuwaongezea thamani wafugaji.