Mkurugenzi wa Me and Orphan Tanzania Musa Mofuga akimkabidhi mgeni rasmi Mhandisi David Mtunguja Cheti Cha kumtambua katika hafla ya kutimiza mwaka mmoja wa Shirika hiloMkurugenzi na Mwanzilishi wa Shirika la Me and Orphan Tanzania ndugu Mussa Mofuga akizungumza katika hafla ya kutimiza mwaka mmoja wa Shirika hiloBaadhi ya wanachama wa Shirika la Me and Orphan Tanzania wakiwa katika Hafla ya kutimiza mwaka mmoja wa Shirika hilo lenye makao take makuu Jijini ArushaBaadhi ya Wagenj waalikwa katika hafla hiyo wakifuarahia Jambo Baadhi ya wenyeviti wa Taasisi binafsi walioshiriki katika hafla hiyo ya kutimiza amwaka mmoja kea Shirika la.Me and Orphan Tanzania lenye makao take makuu Jijini Arusha
Na.Vero
Ignatus,Arusha
Uelewa mdogo wa jamii katika huduma za Mashirika yasiyo
ya Kiserikali, imepelekea kuleta ugumu na
kutoonyesha ushirikiano katika utendaji kazi, katika
kufikia malengo yao kama inavyotakiwa
Musa William Mofuga ni mwanzilishi na Mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilo
la kiserikali linaloitwa Me and Orphans
Tanzania, lenye makao makuu yake mkoani Arusha, anasema lengo kuu la shirika hilo ni
kupata jamii yenye huruma ,utu kwa watoto yatima, na watoto wa mitaani, katika kuwapatia malazi,elimu na masuala ya afya
Alisema Taasisi hiyo inashirikiana na serikali kuibua
changamoto zilizopo katika jamiii,na kusaidia kupata tarifa muhimu ambazo
wakati mwingine zinakuwa hazijasikika mahali pengine .ili kuzipatia ufumbuzi na
kuziwasilisha kwenywe vyombo vinavyohusika kwaajili ya utatuli zaidi.
Mofuga alisema
kuwa dhamira yao kuu ni kuwasaidia
watoto yatima katika jamiii ,kwa kupitia kutoa elimu kwa jamiii, na kwa michango
ya wadau wa maendeleo ya jamii, ili watoto yatima waweze kupata mahitaji ya
msingi na kuhakikisha usalama wao.
Alisema kuwa wanasaidia kuibua chamgamoto zilizopo ndani
ya jamii, zinazochangiwa na mila nadesturi mbaya, ambazo ni kandamizi kwa kutoa
elimu kwa kupitia warsha,semina na vyombo vya habari walau kupunguza changamoto
hizo
Aidha mwanzilishi
wa shirika hilo alisema changamoto kubwa wanazokabiliana nazo kwa sasa ni kukosa pesa za kutosha, na kupelekea
kuelekeza nguvu kubwa kwa michango ya ada za wananchama, na viongozi jambo
ambalo halijaweza kufanikiwa kwa asilimia kubwa
Hivyo basi
Kutokana na hali hiyo imepelekea shirika hilo kukosa ofisi yake ya
kujitegemea ,na kuwalazimu kutumia ofisi ya kampuni fulani ambayo waliiazima kwa
muda ,na kila kitu kilichomo kwenye ofisi hiyo kinakodishwa na ada yake ni
kubwa.
Aidha ameiomba jamii kutambua kuwa uwepo wa mashirika
hayo binafsi, lengo kubwa ni kushirikiana
na serikali kuibua changamoto mbalimbali
za kijamii na kuzitafutia ufumbuzi,kuhakikisha kuwa jamiii inapata unafuu
katika changamoto hizo,kwahi serikali peke yake haiwezi kutekeleza mambo yote
Ameainisha shauku yake kwa kusema kuwa kwa uongozi
utakaoingia madarakani ujitahidi kuwa karibu na taasisi hizo binafsi, kwani
zinafanya kazi kubwa za kuibua changamoto ndani ya jamii,lakini wanapopata
changamoto katika utendaji kazi wao,hawana mahali sahihi pa kupata majibu ya
maswali yao,na hiyo ni kutokana na
kutokuwa na uwazi baina ya mashirika ya siyo ya kiserikali na uongozi unaokuwa
madarakani
Amesema kuwa
shirika hilo lenye wanachama hai wapatao 36 kutoka mikoa mbalimbali nchini ,
ndiyo wanaojitolea kwa kiasi kikubwa katika mapato ya ndani ya sughuli za
shirika hilo, ambapo wameweza kutoa misaada ya vyakula,mavazi,na kudhamini
baadhi ya watoto, katika maeneo ya Arusha mjini kata ya Elerai
,wilaya ya Arumeru,wilaya ya ngorongoro,Oldonyosambu mtaa wa namelok na mtaa wa
Oldonyowasi
Shirika hilo la Me and Orphan Tanzania limesajiliwa kiserikali kwa namba 00NGO/R/00361,ambapo wana jumla ya watoto yatima 20 waliopokatika shirika hilo kwenye kituo chao kulichopo Oldonyosambu Mkoani Arusha.