Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT), Wilaya ya Dodoma, Diana Madukwa akizungumza na wanawake wa Kata ya Nghong’onha wakati wa ziara ya kusaka kura Kata kwa Kata za ushindi Mgombea urais John Magufuli, Mgombea wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde na madiwani wote wa CCM Kata 41.
Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT), Wilaya ya Dodoma, Diana Madukwa,akimuombea Kura mgombea udiwani Kata ya Nghong’onha Mwl.Loth Loth wakati wa ziara ya kusaka kura Kata kwa Kata za ushindi Mgombea urais John Magufuli, Mgombea wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde na madiwani wote wa CCM Kata 41
Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT), Wilaya ya Dodoma, Diana Madukwa,akimtambulisha mgombea udiwani wa viti Maalum Tarafa ya Kikombo alipokuwa amefanya ziara ya kuzungumza na wanawake wa Kata ya Nghong’onha kusaka kura Kata kwa Kata za ushindi Mgombea urais John Magufuli, Mgombea wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde na madiwani wote wa CCM Kata 41
Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT), Wilaya ya Dodoma, Diana Madukwa akiwa na Timu ya ushindi wakiwa wamepiga magoti kumuombea kura kwa wanawake Mgombea udiwani wa Kata ya Nghong’onha wakati wa ziara ya kusaka kura Kata kwa Kata za ushindi Mgombea urais John Magufuli, Mgombea wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde na madiwani wote wa CCM Kata 41
Mgombea udiwani Kata ya Nghong’onha Mwl.Loth Loth ,akiomba kura kwa wanawake wa kata hiyo za ushindi Mgombea urais John Magufuli, Mgombea wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde na madiwani wote wa CCM Kata 41
Baadhi ya wanawake wa Kata ya Nghong’onha wakimsikiliza Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT), Wilaya ya Dodoma, Diana Madukwa,alipokuwa akizungumza na wanawake hao kusaka kura Kata kwa Kata za ushindi Mgombea urais John Magufuli, Mgombea wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde na madiwani wote wa CCM Kata 41
Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT), Wilaya ya Dodoma, Diana Madukwa,akizungumza na wanawake wa Kata ya Ntyuka alipokuwa amefanya ziara ya kuzungumza na wanawake wa Kata ya Ntyuka kusaka kura Kata kwa Kata za ushindi Mgombea urais John Magufuli, Mgombea wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde na madiwani wote wa CCM Kata 41
Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT), Wilaya ya Dodoma, Diana Madukwa,akimuombea Kura mgombea udiwani Kata ya Ntyuka Bw Yona Mambala wakati wa ziara ya kusaka kura Kata kwa Kata za ushindi Mgombea urais John Magufuli, Mgombea wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde na madiwani wote wa CCM Kata 41.
Mjumbe kamati maalum ya ushindi Sella Mkisi,akiomba kura kwa wanawake wa Kata ya Nghong’onha na Ntyuka kwa ajili ya kupata kura za kishindo kwa Mgombea Urais,Ubunge na Madiwani wote wa CCM kwa Kata 41 za Dodoma mjini
…………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
WANAWAKE Wilaya ya Dodoma Mji wamethadharishwa kuwa wasikubali kutokubali kutoa vitambulisho vyao vya kupigia kura kwa watu wanaopita kwenye maeneo yao wakiahidi kuwapatia mikopo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT), Wilaya ya Dodoma, Diana Madukwa alipokuwa akiwaombea kura za ushindi Mgombea urais John Magufuli, Mgombea wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde na madiwani wote wa CCM kwa wanawake wa kata ya Nghong’onha na Ntyuka.
Madukwa amesema kuwa kuna watu wameanza kupita wanachukua vitambulisho hivyo wakiahidi kuwapatia mikopo jambo ambalo si kweli kwa kuwa wamekuwa wakichukua na kwenda kutengeneza nakala inayofanana na kitambulisho hicho.
“Hawa wanachukua na kwenda kutoa ‘copy’ ambayo inakuwa ngumu kama kitambulisho, siku ya kwenda kupiga kura unakuta tayari ulishapiga kura kumbe hujapiga, ndugu zangu msikubali kuwapa watu hao wanaokusanya vitambulisho kitambulisho ni haki yako wewe kwa hiyo nawakumbusha mkatunze vitambulisho vyenu,”amesisitiza
” Dodoma sisi tumefaidika sana na Dk Magufuli kwanza ametuheshimisha kwa kuleta Makao Makuu ya Nchi hapa, wizara zote na taasisi ziko Dodoma hii ni fursa kubwa sana kwetu, ametujengea soko na stendi kubwa ambayo itakuwa chanzo cha mapato kwa Jiji letu, niwaombe Oktoba 28 mjitokeze kwa wingi mkapige kura”amesema Madukwa
Hivyo nawaomba wanawake mjitokeze kwa wingi Oktoba 28 mkiwa na vitambulisho vyenu vya mpiga kura ili Muweze kumchagua mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, Mbunge wa Jimbo hilo Anthony Mavunde na madiwani wote wa kata 41 za Dodoma Mjini.
Aidha, amewaomba wanawake hao kumchagua Rais Magufuli kwa kishindo kwa kuwa ameipaisha Dodoma kwa kuhamishia Makao Makuu ya Nchi.
“Mchague Mavunde kwa maendeleo ya jimbo la Dodoma mjini, lakini hakuna asiyemjua Rais Magufuli ameipenda Dodoma na ulimwengu mzima unafahamu, ukitaja Dodoma unataja moyo wa Magufuli,”amesema Madukwa
Alieleza kuwa mwaka 1973 Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alisema Makao Makuu yawe Dodoma lakini hayakuletwa kwa miaka 47, lakini baada ya kuingia madarakani Rais Magufuli yamehamia ndani ya mwaka mmoja.
Aidha Madukwa amewaomba wanawake wa Kata ya Nghong’onha na Ntyuka kutumia ushawishi wao kuhakikisha wanampigia kura nyingi mgombea huyo wa chama cha mapinduzi Dk.John pombe Magufuli kwa kuwa anauwezo wa kuliongoza taifa hili kimaendeleo kuliko wagombea wengine.