***********************************
Watafiti wa elimu kwenye Demokrasia Tanzania (REDET) watashiriki kikamilifu kuhakikisha uchaguzi Mkuu unakuwa wa haki na uwazi ili kila mtu ama chama kiweze kupata haki ya inayostahili.
Ameyasema hayo leo Mwenyekiti wa REDET, Prof.Rwekeza Mukandala leo katika kikao cha Waandishi wa habari kilichofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaaam.
Akizungumza katika kikao hicho Prof.Mkandala amesema katika kutekeleza haki katika Uchaguzi Mkuu Tanzania Bara na Visiwani wataangalia na kupima uhalali,usawa na haki kwenye uchaguzi huo.
Aidha Prof.Mkandala amesema watahakikisha wanaangalia namna ya vyombo vya utawala hasa NEC na ZEC zinafanya kazi zake kama kweli vinatenda haki kwa wahusika.
“Tunataka kupima sheria za uchaguzi na maelekezo kadhaa ambayo yatakuwa yametolewa kama ni halali na yanakuza na yakulea uhuru na haki na kuangalia pia vyombo vyote vinavyohusika katika Uchaguzi, jeshi la polisi msajili wa vyama vya siasa na wengine wote wanaohusika kwa njia moja ama nyingine katika kufanikisha zoezi hili la uchaguzi”.Amesema Prof.Mkandala.