********************************
NJOMBE
Baada ya wakulima wa zao la mahindi kulia na changamoto ya soko kwa kipindi kirefu , hatimae shirikisho la vyama vya ushirika Afira Mashariki EAFF limeanzisha mradi wa FO4ACP mkoani Njombe utakaojikita katika utafiti wa changamoto zinazo athiri mnyororo wa thamani katika zao la mahindi.
Mradi huo unaotekelezwa katika baadhi ya nchi za Pasific,Caribian na Africa ikiwemo Tanzania utatekelezwa katika kipindi cha miaka minne kwa ufadhili wa umoja wa Ulaya EU
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi na ripoti ya utafiti wa mnyororo wa thamani katika zao mahindi katibu tawala mkoa wa Njombe Katarina Revokati amesema mradi huo umependekezwa kutekelezwa katika eneo sahihi kawa kuwa mkoa wa Njombe umekuwa na kiwango kikubwa cha uzalishaji wa mahindi lakini changamoto ya soko ndiyo kikwazo kwa wakulima.
Kuhusu mnyororo wa thamani ripoti ya utafiti inanyesha kuna changamoto kubwa ya matumizi mbolea na kilimo cha umwagiliaji jambo ambalo limesababisha kushuka kwa ubora na kiwango cha uzalishaji na kwamba ujio wa mradi huo utasaidia kuwaunganisha wakulima,kutatua changamoto ya soko na kutoa elimu, Kama ambavyo ambavyo Teresia Chitumbi mwenyekiti wa shirikisho la vyama ushirika Tanzania TFS na Mtafiti Edwin Mkwela wanasema .
Nao baadhi ya wakulima na wadau wa kilimo wakieleza hali halisi katika kilimo cha mahindi na soko akiwemo Samson Gunda ,Maria Chaula na Samwel Mulumba wanasema uzalishaji ni mkubwa lakini soko limeendelea kukwamisha jitihada za wakulima hivyo wanamatumaini na mradi huo kuja kuwa muarobaini kwao katika soko na ubora
Njombe huzalisha zaidi ya tani laki 5 kila mwaka za mahindi