Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar – Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiashiria utoaji fedha kwa kutumia kadi ya Union Pay katika ATM ya NMB wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo visiwani Zanzibar leo. Wanaoshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki Ya NMB, Ruth Zaipuna (wapili kushoto), Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi (wapili kulia) na viongozi wengine wa Benki hiyo.
Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar – Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (wapili kulia) na viongozi wa Benki ya NMB wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Bi. Ruth Zaipuna wakionesha nembo mpya ya NMB Pay.
Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar – Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiteta jambo na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (kushoto).
***************************************
Benki ya NMB leo imezindua Rasmi huduma mbili za kuongeza ufanisi katika sekta ya utalii nchini. Huduma zilizozinduliwa leo ni pamoja na ushirikiano kati yake na kampuni ya kimataifa ya kadi – Union Pay International (UPI) Kwa lengo la kutoa nafasi kwa watumiaji wa kadi za UnionPay kufanya miamala kwenye mashine za kutolea fedha (ATM) na POS za benki ya NMB. Mbali na ushirikiano huo, benki ya NMB pia imezindua jukwaa la biashara litakalowezesha wafanyabiashara kufanya miamala kupitia tovuti zao (E-Commerce Platform).
Kwa uzinduzi huu, wafanya biashara na makampuni ya huduma yatawezeshwa kupokea malipo kimtandao kupitia tovuti zao, bila ulazima wa wateja kutembelea sehemu za biashara zao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Ruth Zaipuna amesema kuwa ushirikiano na UPI utaleta unafuu na uharaka wa kufanya miamala kwa watumiaji wa kadi za UPI watakao kuwa wanapata huduma kwenye mtandao wa ATM na POS wa NMB muda wowote.
“Hii ni hatua muhimu sana katika kuleta huduma bora kwa wateja wetu, ni fursa pia kwa wafanya biashara hasa wa sekta ya hoteli, maduka na utalii kwa ujumla katika kuwezesha biashara ya kimataifa kupitia malipo mtandao yanayowezeshwa na benki ya NMB,” alisema.
Bi Zaipuna aliongeza kuwa “Kwa mtandao wetu wa zaidi ya POS 1,750 POS na ATM Zaidi ya 800 nchini, huduma hii inategemewa kuleta mapinduzi katika matumizi ya kadi kwa watumiaji wa kadi za UnionPay.”
“Kadi za UnionPay zinajulikana kama nyenzo muhimu ya malipo kwa kufanikisha biashara, utalii na muingiliano wa kiutamaduni kati ya bara la Afrika na Asia. Ushirikiano huu kati ya benki ya NMB na UnionPay International utaongeza matumizi ya kadi za UnionPay nchini na katika miamala ya kimataifa na inaashiria mapinduzi ya teknolojia ya malipokupitia kadi” alisema Meneja Mkuu wa UnionPay International tawi la Afrika – Luping Zhang “tuna furaha kushirikiana na benki kubwa ya NMB kuleta huduma hii muhimu kwa sekta ya utalii Tanzania”.
UnionPay International inatoa huduma za hali ya juu hususani kufanikisha miamala ya kimataifa, iliyo nafuu na salama zaidi kwa watumiaji wa kadi za UnuinPay duniani na pia kuhakikisha uongezekaji wa watumiaji wa kadi za UPI.
Leo, tukiwa na zaidi ya kadi bilioni 8.4 zilizopo katika nchi 61 duniani, UPI inajivunia kuwa kampuni kubwa zaidi ya kadi duniani.
Kwa bara la Afrika, ipo katika nchi 50 huku nchi 11 zikitoa kadi ndani ya nchi zao. Pia UnionPay imezindua huduma mbalimbali za malipo barani Afrika katika kuendana na mabadiliko ya kidigitali na pia ushirikishwaji wa jamii katika huduma za kifedha.
Kadi hizi za Union Pay zitasaidia kuongeza wigo wa mauzo na malipo ya watalii nchini, kwani kabla ya hapo malipo mengi yalifanyika nje ya nchi na hivyo kulikosesha taifa mapato yatokanayo na biashara ya utalii.
Kadi hizi pia pamoja na mtandao mpana wa ATM na POS za Benki ya NMB vitaleta usalama wa fedha za watalii kwani hawatalazimika kutembea na fedha taslimu