Maafisa kutoka Shirika la Viwango Tanzania TBS wakikagua bidhaa za Vipodozi kwenye moja ya maduka waliyoweza kutembelea Magomeni Jijini Dar es Salaam ma kubaini baadhi ya bidhaa hizo hazijakidhi viwango
*************************************
NA EMMANUEL MBATILO
Shirika la Viwango Tanzania TBS limefanikiwa limefanya msako wa kushtukiza katika baadhi ya maduka ya vipodozi Magomeni Jijini Dar es Salaam na kufanikisha kukamata baadhi ya vipodozi ambavyo havijakidhi viwango.
Akizungumza baada ya ukaguzi Afisa Udhibiti Ubora TBS Bi.Mbumi Mwampeta amesema katika ukaguzi walioufanya wamegundua baadhi ya bidhaa ambazo zimeshakatazwa lakini bado zipo sokoni na nyingine nyingi wamezibaini hazina taarifa ya uzalishaji na mwisho wa matumizi.
“Tumegundua bidhaa ambazo zilikatazwa na bado zipo Sokoni na kuna bidhaa zingine tumezigundua katika lebo hazina taarifa ya uzalishaji na mwisho wa matumizi ya bidhaa lakini pia tumegundua lugha ambazo hazitakiwi kutumika kwenye soko kwasababu hazieleweki kwa mtumiaji wa kawaida”.Amesema Bi.Mbumi.
Aidha amesema kuna lugha ambazo zinatakiwa kutumika kwenye lebo ya bidhaa ambazo ni zile lugha za Afrika Mashariki ikiwemo Kiingereza, Kiswahili na Kifaransa.
Pamoja na hayo amewataka wafanyabiashara watembelee tovuti ya TBS kufahamu ni bidhaa gani ambazo hazitakiwi kuwa sokoni ili kuondokana na usumbufu utakaojitokeza na kumgharimu.
Hata hivyo amewataka waingizaji wa bidhaa za vipodozi na vyakula nchini kufila TBS ili waweze kusajili bidhaa zao kwaajili ya usalama wake.