MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha uuzaji wa madini
Kalalani wilayani Korogwe kulia Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe (DAS) Rahel Mhando kushoto ni
Mwenyekiti wa Chama cha
Wachimbaji Madini Wanawake Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo
akifuatiwa na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho na kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe Rahel Mhando
Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo cha uuzaji wa madini |
Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo akisisistiza jambo wakati wa uzinduzi wa kituo cha ununuzi wa madini Kalalani wilayani Korogwe |
Katibu wa Tawoma Salma Kundi akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Katibu
Tawala wa wilaya ya Korogwe Rahel Mhando akieleza jambo wakati wa
uzinduzi huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa na kulia
ni Katibu wa Tawoma Salma Kundi
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo wa kituo cha Ununuzi wa Madini Kalalani Korogwe |
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi huo wa kituo cha Ununuzi wa Madini Kalalani Korogwe katikati ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa na kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe Rahel Mhando na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo na wa kwanza kulia ni Katibu wa Chama hicho Salma Kundi |
Shughuli za utambuzi wa madini zikiendelea wakati wa uzinduzi wa kituo cha kuuzia madini Kalalani wilayani Korogwe kama inavyoonekana |
Shughuli za utambuzi wa madini zikiendelea wakati wa uzinduzi wa kituo cha kuuzia madini Kalalani wilayani Korogwe kama inavyoonekana |
MKUU
wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa katikati akiwa na Afisa Madini Mkazi
wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho kulia na Mwenyekiti wa Tawoma Eunice Negelo kushoto wakionyeshwa aina mbalimbali madini
MKUU wa wilaya ya
Korogwe Kissa Gwakisa katikati akiwa na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa
Tanga Zabibu Napacho kulia na Mwenyekiti wa Tawoma Eunice Negelo kushoto wakionyeshwa aina mbalimbali madini
MKUU
wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa katika akipata maelekezo kushoto ni
Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe Rahel Mhando akifuatiwa na Afisa
Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho
MKUU
wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Kissa Gwakisa amewaonya wachimbaji wa madini
wenye tabia ya kutorosha madini waache mara moja badala yake wafuateni taratibu
zilizowekwa na Serikali.
Kissa
aliyasema hayo wakati akifungua kituo cha uuzaji Madini eneo la Kalalani
wilayani Korogwe ambapo alisema serikali inaruhusu mtu kuuza madini sehemu
yoyote anapotaka lakini tabia ya utoroshaji haitakiwa na wasijaribu kufanya
hivyo.
Katika
ufunguzi wa kituo hicho kilihudhuria na Afisa Madini mkazi wa Mkoa wa Tanga
Zabibu Napacho na maafisa wengine wa ofisi na Mwenyekiti wa Chama cha
Wachimbaji Madini Wanawake Tanzania (Tawoma) Eunice Negelo wakiwemo wauzaji na
wanunuzi.
Alisema lazima wachimbaji kubadilika na kuacha
na tabia za namna hiyo kwa kuhakikisha wanafuata taratibu zilizokwekwa kwa
mujibu wa sheria kuweze kuwa na manufaa kati ya wachimbaji, serikali na jamii
kwa ujumla.
“Labda
niwaambie kwamba Mkuu wa Polisi wilaya ya Korogwe (OCD) ndio atakuwa na jukumu
la kulinda kituo hiki kipya ambacho kinaanzishwa hapa cha ununuzi na uuzaji
pamoja na jeshi la akiba watoe vijana kila siku ya soko ambao watakuja kuwasindikiza
wanunuzi mpaka watakapotoka nje ya wilaya hiyo na ndio maana kamati ya ulinzi ipo
hapa”Alisema DC Kissa
Aidha
alibainisha kwamba kwenye wilaya hiyo wana jumla ya leseni za wachimbaji 153
lakini zinazooneka na zinafanya kazi ni 25 hivyo uanzishwaji wa kituo hicho
utakuwa ni kuchochea cha wale wenye leseni ambazo hawafanyi kazi kufanya kazi
ili leseni hizo ziweze kuleta tija kwa wananchi wa wilaya ya Korogwe na
wanunuzi,.
“Lakini
pia niwaambie kwamba tunafikiria kuanzisha kituo kikubwa Korogwe mjini cha Soko
la Madini ni mipango wanaendelea nayo na tunaamini utakuwa na tija hivyo na
kuwawezesha wachimbaji kuuza madini yao “Alisema
Mkuu
huyo wa wilaya alisema kwamba anaamini jambo linalofanyika halijakiuka sheria
za nchi na limefuata miongozi hivyo ni vuzuri uendeshaji wake na jinsi soko
litakavyokuwa linakwenda lifuate sheria ili serikali iweze kupata manufaa yake
na wananchi mtu mmoja mmoja waweze kupata na wanunuizi wanaokwenda kununua
wasijutie uanzishwaji wake.
“Tunatambua
tunao brokers ambao wanakuja kununua madini kwa wachimbaji wadogo naawaomba
sana wasimamizi hapo, ofisi ya madini mkoa ambayo ipo chini ya wizara ya madini
watusaidie kuangalia kwamba kunakuwa na uwanja uliopo sawa kwa ajili ya watu
wote kati ya muuzaji na mnunuzi ili soko hilo liweza kuwa na maisha
marefu”Alisema
Alisema
kwa sababu ikitokea mmoja analalamika au kuna upande unaumizwa soko litakuwa
halina maisha marefu huku akieleza kituo hicho hatakuwa cha madini yanayotoka
kalalani pekee bali madini yote ya vito yanayotoka wilayani humo yatauzwa hapo.
“Kama
mtakumbuka Serikali chini ya Rais Dkt John
Magufuli ilianzisha masoko na vituo vya uuzwaji wa madini kwenye maeneo
mbalimbali hapa nchini na nyie wenyewe mmeshughudia RC Martine Shigella amekwisha
kuzindua masoko mawili Handeni na Mkinga leo ni muendelezo wa yake masoko na
vituo vilivyoanzishwa rasmi kwa miongozo na maelekezo wa Rais “Alisema
“Tunafungua
tukifuatia kifungu cha sheria namba 17 cha sheria ya madini ya mwaka 2010
ambayo imekuwa ikifanyiwa marekebisho mwaka 2017,2018 na 2019 na kanuni zake za uanzishwaji wa masoko lakini
pia niwapongeze Tawoma,Tarema na wadau Moyo Gems kwa juhudi kubwa mnazozifanya”Alisema
Awali
akizungumza katika ufunguzi huo Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu
Napacho aliwataka wachimbaji wa madini kuhakikisha wanafuata taratibu na sheria huku akieleza wadau wa kalalani watauza madini
yao hapa hapo kwenye kituo hicho.
Naye
kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Wanawake Tanzania
(Tawoma) Eunice Negelo alisema wana mshukuru Rais Dkt John Magufuli kwa jinsi
alivyowasaidia wanawake wachimbaji kwa kuweza kuwathamini,kuwaamini na kuwawezesha
na wameweza kufanya miradi mbalimbali wakiwa huru na amani kwa sababu ya
uongozi wake bora.
“Kwa
kweli tunamshukuru Rais Dkt John Magufuli kutokana na kuwathamini na kuwaelewa
wachimbaji leo hii tumeweza kuuza madini kwa uhuru na amani na lakini pia uwepo
wa masoko ya madini yaliyoanzishwa na wakina mama Tawoma wakiungana na Chama
cha Pact na kuzalisha kitu kinachoitwa Moyo Gems”Alisema Mwenyekiti huyo.