Kiongozi wa Sungusungu wa kijiji hicho, Nking Pagi, akizungumza kwenye mkutano huo.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mwamalili, Wallacee Kiondo, akizungumza kwenye mkutano huo.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Mondo, Masanja Said, akizungumza kwenye mkutano huo.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ng’wigumbi, Barbara Ndetabura, akizungumza kwenye mkutano huo.
Fundi Sanifu wa Umeme na Vifaa vya Umeme wa Wakala wa Maji Safi na Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Kishapu, Christopher Damas, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkazi wa Kijiji cha Buchambi, Ngussa Hussein, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mhandisi kutoka Kampuni ya Williamson Diamonds Limited, akizungumza kwenye mkutano huo.
,
Afisa Uvuvi kutoka Wilaya ya Kishapu. Moses Zacharia, akizungumza kwenye mkutano huo.
Afisa Mahusiano na Maendeleo wa Kampuni ya Williamson Diamonds Limited, Gamba Mtoni, akizungumza na wananchi hao.
Wakina Mama wa Kijiji cha Buganika wakiwa kwenye mkutano.
Dotto Mwaibale na Godwin Myovela , Shinyanga.
BODI ya Maji Bonde la Kati kwa kushiriana na viongozi wa vijiji na kata ambao ni wawakilishi wa wananchi wanaotumia Bwawa la Nhumbu wamefanikiwa kuanzisha jumuiya ya watumia maji kwa ajili ya kuhifadhi vyanzo vya maji mkoani Shinyanga.
Akizungumza jana kuhusu huanzishwaji wa jumuiya hiyo Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi wa Bodi ya Maji Bonde la Kati, Nelea Bundala alisema jumuiya hiyo itasaidia kulinda vyanzo vya maji ambavyo vinaharibiwa kutokana na shughuli mbalimbali zikiwemo za kilimo zinazofanyika mpaka ndani ya bwawa hilo.
Alisema kwa kuwa wao kazi yao kubwa ni kusimamia rasilimali za maji ili ziwe endelevu kwa vizazi vilivyopo na vijavyo wameona ni muhimu kuwepo na jumuiya ya watumia maji hususani kwa kuanzia Bwawa la Nhumbu na baadae Bwawa la Songwa na mengine ili kuhakikisha yanadumu na wanayatumia kwa mujibu wa sheria zilizopo.
Bundala alisema sheria inaelekeza kwamba mtumiaji wa maji ndiye mtunzaji namba moja wa maji kwa sababu ni mnufaika na yupo maeneo ya vyanzo vya maji husika.
Alisema wametembea kwenye vijiji hivyo na kufanya mikutano na kupata wawakilishi watatu kutoka katika kila kijiji wakiwakilisha kundi la wafugaji, wakulima na watumiaji wa maji na kuwa sasa wanamalizia mchakato kwa kukamilisha kuunda jumuiya hiyo baada ya kutoa mafunzo ya siku tatu ili waweze kujua sheria na sera ya maji inasemaje na majukumu yao ya kusimamia rasilimali ya maji.
Alisema mchakato huo ume wamewashirikisha viongozi wa vijiji kwa sababu wao ni walinzi wa amani, wasimamizi wa kuu ngazi za vijiji hivyo jumuiya haiwezi kufanya kazi peke yake bila ya kushirikiana na vijiji.
“Viongozi wa vijiji pamoja na wawakilishi wa vijiji kwa pamoja tumekaa darasani tukiamini tutakuwa na uelewa wa pamoja tukianzia kwa viongozi na wana jumuiya wenyewe wanaozunguka mabwawa hayo.” alisema Bundala.
Bundala alisema katika mchakato huo wamewashirikisha wadau wengine kama Williamson Diamonds Limited wanao miliki Mgodi wa Almasi wa Mwadui na Bwawa la Nhumbu, Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Manispaa ya Shinyanga, Mwakilishi kutoka Ofisi ya Meneja wa Maji Safi na Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Kishapu lengo likiwa kuunda jumuiya hiyo ambayo itakuwa ikisimamia rasilimali za maji katika maeneo hayo.
Alisema baada ya hapo wajumbe watakuwa na katiba na mpango kazi na rasimu ya katiba ambayo watarudi nayo vijijini na kuipitisha kwa wananchi ili waielewe kabla haijawa katiba rasmi na hatimaye wataizindua jumuiya hiyo ili iweze kufanya kazi yake.
Alisema lengo ni kuhakikisha kama wizara ya maji wadau wanaielewa sera , sheria na kuunda vyama vya watumia maji viweze kuhakisha vinafanya kazi kwa niaba ya bonde kusaidia wizara kutunza mazingira na vyanzo vya maji.