Home Mchanganyiko WANANCHI WANA IMANI KUBWA NA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI*

WANANCHI WANA IMANI KUBWA NA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI*

0

*******************************

Na Mwandishi wetu Mihambwe
Wananchi wameendelea kuwa na imani kubwa na mfumo wa stakabadhi ghalani kwa kuendelea kupeleka mazao yao. 
Wananchi mbalimbali wameonekana wakipeleka Korosho zao kwenye maghala ya vyama vya msingi ikiwa siku chache tangu msimu wa Korosho 2020/2021 kufunguliwa.
Hayo yamejitokeza kwenye ziara ya Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu wakati akitembelea Maghala mbalimbali ili kujiridhisha na utaratibu unaotumika ambapo ameshuhudia Maghala yamefunguliwa na Wakulima wanapeleka Korosho zao ghalani.
“Nimefanya ziara kutembelea Maghala mbalimbali, nimejionea imani kubwa ya Wananchi juu ya mfumo wa stakabadhi ghalani kwa kupeleka Korosho zao ghalani, uwingi wa Korosho kwenye Maghala ni vitendo vinaongea vya Wakulima. Nawasihi Wananchi wazidi kuleta mapema Korosho zao ili wawahi minada ya awali ambayo mengi kihistoria yanaonekana kuwa na bei kubwa. Kadri wanavyowahi kupeleka Korosho zao ghalani ndivyo wanavyojiweka kwenye mazingira rafiki kupata bei kubwa na fedha kwa wakati.” Alisema Gavana Shilatu.
Pia Wakulima wameiomba Serikali kuendelea kusimama nao pamoja ili masoko ya Korosho zao yapatikane kwa haraka na kwa bei nzuri.
“Nimepima Korosho zangu hapa ghalani, Kuna mwitikio mzuri kwa Wakulima kuleta Korosho zao na zinapatikana. Tunaomba Serikali itusimamie tupate haki zetu kwa wakati na kwa  bei nzuri.” Alisema Ismail Mohammed Namkoma mkazi wa kijiji cha Namunda.
Msimu wa Korosho 2020/2021 umefunguliwa tayari na Wakulima wanapeleka Korosho zao ghalani tayari kusubiri minada.