Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Balozi wa Uswiss nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot, wakisaini Mikataba miwili ya msaada wa Faranga za Uswis milioni 17.8 sawa na Sh. bilioni 44.1 kwa ajili ya kugharamia Awamu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) kwa mwaka 2020-2023 na Mkataba wa Mfuko wa Pamoja wa Afya kwa mwaka wa fedha 2020/21, hafla iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Balozi wa Uswiss nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot, wakibadilishana Mikataba miwili ya msaada wa Faranga za Uswis milioni 17.8 sawa na Sh. bilioni 44.1 kwa ajili ya kugharamia Awamu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) kwa mwaka 2020-2023 na Mkataba wa Mfuko wa Pamoja wa Afya kwa mwaka wa fedha 2020/21,hafla hiyo imefanyika leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Balozi wa Uswiss nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot,wakionesha Mikataba miwili ya msaada wa Faranga za Uswis milioni 17.8 sawa na Sh. bilioni 44.1 kwa ajili ya kugharamia Awamu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) kwa mwaka 2020-2023 na Mkataba wa Mfuko wa Pamoja wa Afya kwa mwaka wa fedha 2020/21,hafla hiyo imefanyika leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James,akizungumza mara baada ya kusaini Mikataba miwili ya msaada wa Faranga za Uswis milioni 17.8 sawa na Sh. bilioni 44.1 kwa ajili ya kugharamia Awamu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) kwa mwaka 2020-2023 na Mkataba wa Mfuko wa Pamoja wa Afya kwa mwaka wa fedha 2020/21 hafla hiyo imefanyika leo jijini Dodoma.
Balozi wa Uswiss nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot,akizungumza mara baada ya kuipatia Tanzania msaada wa Faranga za Uswis milioni 17.8 sawa na Sh. bilioni 44.1 kwa ajili ya kugharamia Awamu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) kwa mwaka 2020-2023 na Mkataba wa Mfuko wa Pamoja wa Afya kwa mwaka wa fedha 2020/21,hafla iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini Mikataba miwili ya msaada wa Faranga za Uswis milioni 17.8 sawa na Sh. bilioni 44.1 kwa ajili ya kugharamia Awamu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) kwa mwaka 2020-2023 na Mkataba wa Mfuko wa Pamoja wa Afya kwa mwaka wa fedha 2020/21,hafla iliyofanyika leo jijini Dodoma.
………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Uswisi zimesaini makubaliano ya mikataba miwili ya msaada ya Jumla ya shilingi bilioni 44.1 itakayojikita katika miradi ya maswala ya kijamii.
Akizungumza mara baada ya kusainiana mikataba hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Doto James, amesema kati ya fedha hizo bilioni 39.15 itagharimia awamu ya pili ya mpango wa kunusuru kaya maskini chini ya mfuko maendeleo ya Jamii (TASAF) 2020 hadi 2023.
Huku mkataba wa pili kuwa ni wamsaada wa shilingi bilioni 4.95 kwa ajili ya kuchangia mfuko wa pamoja wa afya kwa mwaka wa fedha 2020 hadi 2021.
” Lengo la program hii ni kuboresha upatikanaji wa fulsa kujipatia kipato na huduma za kijamii kwa kaya maskini kulinda na kuboresha nguvu kazi ya familia zisizojiweza
” Na lengo la mpango wa mfuko wa pamoja ni kuimarisha mfumo wa utoaji wa huduma za afya ya msingi ikiwa ni malengo kuboresha huduma za afya kwa jamii” amesema James.
Akizungumzia mradi wa TASAF amesema nchi hizo mbili zimekuwa na ushirikiano tangu mwaka 1960 ambayo inathibitishwa na miradi inayoendelea na iliyokamilika kwa kufadhiliwa na Serikali ya Uswisi.
Amesema msaada huo utasaidia kupunguza umaskini na kuboresha nguvu kazi, kuboresha upatikanaji wa fulsa ya kujipatia kipato kwa kaya maskini na kujenga na kulinda nguvu kazi ya watoto wao, na kuongeza uwezo wa kumiliki mali na huduma za kijamii.
Kuhusu mpango wa TASAF awamu ya kwanza uliotekelezwa kutoka 2013 hadi 2019, ulitelelezwa katika mamlaka za serikali za mitaa 159 bara na visiwani na kuzifikia kaya milioni 1.1 zenye watu milioni 5,296,470 kwa kutoa ajira za mda kwa kaya zenye uwezo wa kufanya kazi.
Ameongeza kuwa” TASAF imeweza kuongeza kipato kwa kaya maskini kupitia kujiwekea akiba na kujihusisha na shughuri za kiuchumi ili kuboresha maisha yao, pia vikundi vya akiba 22,303 vyenye wanavikundi 311,114 viliundwa katika halmashauri 54 za bara na visiwani” amesema.
Akizungumzia programu ya mfuko wa pamoja wa afya utakao wezeshwa kiasi cha bilioni 4.95 amebainisha kuwa Uswisi ni moja ya nchi zinazochangia sana sekta ya afya hapa nchini na kuwa na mafanikio makubwa hasa kwa watanzania maskini.
Amesema tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya awamu ya tano kumekuwa na maboresho makubwa katika sekta ya afya na kumekuwa na ongezeko la vituo vya afya ambapo mwaka 2015 vilikuwa 718 hadi kufikia vituo 1205 kwa mwaka 2020.
Kuongezeka kwa Hospitali za Halmashauri kutoka 77 mwaka 2015 hadi hadi hospitali 178 mwaka 2020 ambapo kunaongezeko la hospitali 101 ziko hatua mbalimbali za ujenzi, kuongezeka kwa zahanati kutoka Zahanati 6,044 hadi kufikia 7,242 kwa mwaka 2020.
Kwa upande wake Balozi wa Uswisi hapa nchini Bw.Didier Chassot amesema ushishirikiano wa nchi hivi mbili ni wa mda mrefu na wataendelea kushirikiana kwa mambo mbalimbali ya kimaendeleo.
” Utafurahi kujua kuwa watendaji kutoka Uswisi walianza kufanya kazi na aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo na baadaye Rais Mwalimu Julius Nyerere katika kuanzisha kati ya vituo vya kwanza vya kutoa huduma ya afya vijijini nchini Tanzania” amesema Balozi Didier.
Aidha amebainisha kuwa nchi ya Uswisi imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuleta mageuzi ya kisekta yanayolenga kuimarisha utoaji wa muhimu kwa watanzania.
” Takribani theruthi mbili ya misaada ya Uswisi imetolewa kuchangia bajeti ya mifuko ya pamoja ya kisekta na karibia theruthi moja katika mipango misaada ya kiufundi pamoja na TAMISEMI, misaada ya kiufundi imechangia kuanzishwa kwa mfuko wa afya ya Jamii CHF iliyoboreshwa na kuendeleza ajenda ya kutokomeza malaria” amesema.
Amebainisha kuwa makubaliano ya leo yataruhusu kuendelea kuchangia mpango wa afya kwa wote (Universal Health Coverage) Tanzania katika mwaka huu wa fedha.