……………………………………………………………………………
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Dkt Tulia Ackson amesema ilani ya Chama chake ni kuleta maendeleo ikiwemo ujenzi wa kivuko cha reli ambacho kinaunganisha Kata za Tembela,Mwasanga na Mbeya Vijijini.
Aidha amesema kupitia Taasisi yake imewezesha kiuchumi kikundi cha Sijali ambacho kimepewa msaada wa shilingi milioni mbili pia kikundi kimeanza kukopesheka.
Hata hivyo alisema binafsi amejitolea shilingi milioni tatu na laki tano kwa ajili ya ujenzi wa kivuko cha muda na kama haitoshi amejitolea kukarabati daraja la muda katika daraja la Mwasanga lililoua watu watano msimu wa masika.
Tulia amewataka kuwachagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi Diwani,Mbunge na Rais ili kuwa na muunganiko utakaoleta maendeleo.
Tulia amesema amejipanga vizuri ili kukamilisha zahanati iliyogharimu zaidi ya shilingi milioni hamsini ambapo inaupungufu wa shilingi milioni ishirini na tatu na laki saba.
Amesema ili kutoa huduma bora za mama na mtoto kupunguza vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano alitoa shilingi milioni arobaini kituo cha afya Ruanda.
Kwa upande wa elimu amejitolea mabati na saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu yaliyogharimu shilingi milioni thelathini na saba.
Ameahidi kuboresha ofisi ya walimu shule ya sekondari Mwasanga.
Amewataka wananchi kuchagua Mbunge anayetulia bungeni pamoja na Rais atakayeleta maendeleo ikiwa ni pamoja na utatuzi wa changamoto ya maji kupitia meadi mkubwa wa maji wa Kiwira.
Kwa upande wa nishati Dkt Tulia amesema kupitia nafasi yake ameweza kuwaombea umeme wa REA ambapo wananchi wanalipa shilingi elfu ishirini na saba.
Amesema serikali imejipanga kuboresha kilimo chenye tija ili mazao watakayolima yapate soko.
Amesema ameanza kutoa bima za afya kwa kaya mbali mbali.