Mshindi wa kwanza aliyeibuka kidedea katika kinyang’anyiro cha wa shindano la kumsaka miss kiteshe 2020 Sarah Zacharia 23 wa kati kati akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa tatu bora, kushoto kwake ni mshindi wa nafasi ya pili Zadia Ally huku kulia kwake mshindi wa tatu Zenat Rajab wakiwa pamoja na viongozi walihudhulia katika shindano hilo.
Mwanadada Sarah Zacharia ambaye ni mshindi wa kwanza katika shindano la miss kiteshe wa kati kati akionyesha ishara ya kumwomba Mungu baada ya kutangwazwa kuibuka kidedea akiwa pamoja na washiriki wengine amabapo kulia kwake ni mshindi wa pili Zenat Rajabu na kushoto kwake ni mshindi wapili Zadia Ally
***********************************
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Mwanadada Sarah Zacharia mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa kwa mathiasi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani ameibuka kidedea baada ya kulitwaa taji la kumsaka miss Kiteshe 2020 huku nafasi ya mshindi wa pili ikianda kwa Zadia Ally (19) na nafasi ya mshindi wa tatu ikinyakuliwa na mwanadada Zenat Rajab.
Kutokana na ushindi huo washindi hao watatu wamepata zawadi mbali mbali kutoka kwa uongozi wa kiteshe pub sambamba na kuchaguliwa rasmi kuwa mabalozi ambao watakuwa na jukumu kwa ajili ya kutangaza mbuga ya Nyerere National park iliyopo Wilayani Rufiji pamoja na vivutia mbali mbali vinavyopatakanika katika eneo hilo.
Katika kinyan’ganyiro cha shindano hilo ambalo lilifanyika mwishoni mwa wiki liliandaliwa kwa ajili ya dhumuni la kuwasaka walimbwende watatu ambao watakuwa na jukumu kubwa la kushirikiana na wadau wengine pamoja na serikali katika kuleta mabadiliko ya kutangaza utalii wa ndani amabo unapatikana katika baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Pwani.
Shindaho hilo ambalo liliwashirikisha washiriki wapatao kumi kutoka maeneo mbali mbali lilikuwa na msisimko na ushindano wa aiana yake kutokana na warembo wote walikuwa wamejiandaa vilivyo katika staili tofauti na mwonekano mzuri wa mavazi yao ambayo yaliweza kuwavutia mashabiki waliofika katika eneo hilo la kiteshe kushuhudia mchuano huo ambao umeweza kuacha historia kwa wakazi wa kibaha.
Pia katika shindano hilo warembo hao waliweza kuulizwa maswali mbali mbali na majaji yanayohusiana na masuala mbali mbali ya utalii pamoja na mambo mengine ya kijamii ili kuweza kuona upeo wao katika sekta ya utalii na baadhi yao waliweza kujibu maswali hao kwa umakini hali ambayo iliwafanya mashabiki waliofika kuweza kupiga mayowe kwa shangwe kulingana na majibu yaliyokuwa yakijibiwa na walimbwende hao.
Kwa uapnde wake Miss Kiteshe Sarah Zacharia amabye ametwaa taji hilo alisema kwamba baada ya kuunyakua ushindi huo lengo lake kubwa ni kuhakikisha anajipanga vilivyo katika kuleta mabadiliko katika kutangaza utalii wa ndani ikiwemo pamoja na kutoa fursa kwa jamii kuwaelimisha umuhimu wa kutembelea mbuga mbali mbali za wanyaama ikiwemo ya Nyerere National Park.
“Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kunifikisha hapa mpaka nimeweza kuchaguliwa kuwa miss kiteshe kwa mwaka huu wa 20202 lakini ndoto yangu kubwa ambayo ninayo ni kuendeleza kufika mbali zaidi ya hapa katika kutangaza mambo mbali mbali ya utalii wa ndani ukizingatia tuna mbuga nyingi ikiwemo ille ya Nyerere National Park,”alisema Sarah.
Pi alitoa wito kwa washiriki wenzake ambao hawakuweza kupata nafasi ya kuibuka kuwa washindi wasikate tama na badala yake wahakikishe wanaendeleza vipaji vyao na fani ya kutangaza utalii wa ndani kupitia fani ya ulimbwende pamoja na kushirikiana vilivyo na wadu wengine ili kutimiza malengo waliyojiwekea.
Nao baadhi ya walimbwende wengine ambnao walishiriki katika kinyanganyiro hicho waliweza kutoa shukrani zao za kipekee kwa Mkurugenzi wa kiteshe Pub kwa kuamua kuandaa shindano hilo kwa lengo la kuweza kutangaza utalii wa ndani kupitia fani ya ulimbwende huku wakiiomba serikali kutoa sapoti katika sekta hiyo ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea.