******************************
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe amekutana na uongozi wa kiwanda cha kutengeneza vigae cha KEDA kilichopo Kibaha mkoani Pwani. Katika kikao hicho Katibu Mkuu amekipongeza kiwanda hicho kwa kuendelea kuzalisha vigae vyenye ubora na akaahidi kutoa ushirikiano pale wanapohitaji. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho ndugu Tonny ameshukuru kwa mazungumzo hayo na Uongozi wa Wizara na akaahidi kuendelea kuzalisha kwa wingi.
Aidha, Katibu Mkuu amezungumza na ndugu Tonny Mkurugenzi wa KEDA ambaye pia ni kiongozi wa Wawekezaji wa China hapa nchini kuona fursa ya kuanzisha kiwanda kipya cha saruji kanda ya ziwa ili miradi mikubwa ya ujenzi inayotekelezwa serikali ipate saruji kwa wakati na kwa bei nafuu.
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu aliambatana na Naibu Katibu Mkuu ndugu Ludovick Nduhiye.
5 Oktoba, 2020