Home Mchanganyiko SHIGONGO ASITISHA KAMPENI KWA BAADA YA MSIBA

SHIGONGO ASITISHA KAMPENI KWA BAADA YA MSIBA

0

………………………………………………………………………………

Mgombea Ubunge Jimbo la Buchosa kupitia Chama Cha Mapinduzi, Eric Shigongo James amesitisha kampeni kwa muda wa saa kadhaa baada ya kupata taarifa ya msiba wa mtoto aliyefariki ghafla katika Kijiji cha Nyanango wakati akiwa kwenye kampeni katika Kijiji cha Nyehunge, Buchosa Mwanza leo Oktoba 4, 2020.

Baada ya kupokea taarifa hizo, Shigongo alielekea moja kwa moja msibani na kuwapa pole ndugu, jamaa na marafiki waliompoteza mtoto wao Kelvin Joel mwenye umri wa miezi tisa.

Imeelezwa kuwa chanzo cha kifo hicho ni baada ya mama mzazi wa mtoto huyo, Bi. Juliana Joel kumlaza kitandani, nyumbani kwake lakini akiwa amelala, mtoto alijigeuza na kuanguka na kubanwa na kitanda na ukuta ndipo aliposhindwa kujiokoa na kupoteza maisha.

Imeelezwa pia kuwa wakati huo mama yake alikuwa nje akiendelea na shughuli zake kwa muda mrefu huku akidhani mtoto Kelvin bado amelala kumbe tayari alibanwa na kushindwa kupumua Kisha umauti ukamfika.

Mungu ailaze Roho ya Marehemu mtoto Kelvin Pema Peponi.. Amen!