Katibu wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Dodoma Mjini (UWT), Diana Madukwa akicheza ngoma na kikundi cha Mbalawala alipofanya ziara ya katika Kata ya Mbalawala kwa ajili ya kuzungumza na wanawake wa Kata ya hiyo ni ziara ya kata kwa kata kwenye vikao vya ndani kusaka ushindi wa CCM.
Katibu wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Dodoma Mjini (UWT), Diana Madukwa akizungumza na wanawake wa Kata ya Mbalawala alipofanya ziara ya kata kwa kata kwa kuzungumza na wanawake wa kata hiyo pamoja na kuelezea mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka mitano ya serikali ya Rais Dkt,John Magufuli na kufanya vikao vya ndani.
Wanawake wa Kata ya Mbalawala wakimsikiliza Katibu wa UWT Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa (hayupo pichani) alipofanya kikao nao kuwaeleza mafanikio ya serikali ya awamu ya tano kwenye awamu ya kwanza ya Rais Magufuli pamoja na kumuombea Kura
Katibu wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Dodoma Mjini (UWT), Diana Madukwa akiwa katika picha ya pamoja na wanawake wa Kata ya Mbalawala alipofanya ziara ya kata kwa kata kwa kuzungumza na wanawake wa kata hiyo pamoja na kuelezea mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka mitano ya serikali ya Rais Dkt,John Magufuli na kufanya vikao vya ndani.
Baadhi ya Wanawake wa kijiji cha Lugalu wakimsikiliza Katibu wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Dodoma Mjini (UWT), Diana Madukwa alipokuwa akizungumza nao katika Kata ya Mbalawala alipofanya ziara ya kata kwa kata kwa kuzungumza na wanawake wa kata hiyo pamoja na kuelezea mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka mitano ya serikali ya Rais Dkt,John Magufuli na kufanya vikao vya ndani.
Katibu wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Dodoma Mjini (UWT), Diana Madukwa akiwahimiza wanawake wa Kata ya Mbalawala alipofanya ziara ya kata kwa kata kwa kuzungumza na wanawake wa kata hiyo pamoja na kuelezea mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka mitano ya serikali ya Rais Dkt,John Magufuli na kufanya vikao vya ndani.
Katibu wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Dodoma Mjini (UWT), Diana Madukwa akicheza ngoma na wanawake wa Kata ya Mbalawala alipofanya ziara ya kata kwa kata kwa kuzungumza na wanawake wa kata hiyo pamoja na kuelezea mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka mitano ya serikali ya Rais Dkt,John Magufuli na kufanya vikao vya ndani.
Katibu wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Dodoma Mjini (UWT), Diana Madukwa akiwa katika picha ya pamoja na wakazi wa Lugalu alipokuwa akizungumza na wanawake wa Kata ya Mbalawala alipofanya ziara ya kata kwa kata kwa kuzungumza na wanawake wa kata hiyo pamoja na kuelezea mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka mitano ya serikali ya Rais Dkt,John Magufuli na kufanya vikao vya ndani.
………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT), Wilaya ya Dodoma, Diana Madukwa,amewataka wanawake kutokubali kutoa vitambulisho vyao vya kupigia kura kwa watu wanaopita kwenye maeneo yao wakiahidi kuwapatia mikopo.
Kauli hiyi ameitoa leo jijini Dodoma wakati akiwaombea kura za ushindi Mgombea urais John Magufuli, Mgombea wa Jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde na madiwani wote wa CCM Kata 41 kwa wanawake wa kata ya Mbalawala.
Madukwa amesema kuwa kuna watu wameanza kupita wanachukua vitambulisho hivyo wakiahidi kuwapatia mikopo jambo ambalo si kweli kwa kuwa wamekuwa wakichukua na kwenda kutengeneza nakala inayofanana na kitambulisho hicho.
“Hawa wanachukua na kwenda kutoa ‘copy’ ambayo inakuwa ngumu kama kitambulisho, siku ya kwenda kupiga kura unakuta tayari ulishapiga kura kumbe hujapiga, ndugu zangu msikubali kuwapa watu hao wanaokusanya vitambulisho kitambulisho ni haki yako wewe kwa hiyo nawakumbusha mkatunze vitambulisho vyenu,”alisema.
Aidha amewaomba wanawake hao kujitokeza kwa wingi Oktoba 28 wakiwa na vitambulisho vyao vya mpiga kura ili waweze kumchagua mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, Mbunge wa Jimbo hilo Anthony Mavunde na madiwani wote wa kata 41 za Dodoma Mjini.