************************************
Na Mwandishi wetu,
Katibu Mstaafu wa halmashauri kuu ya Taifa Siasa na Uhusiano wa kimataifa (Suki) January Makamba amewaomba wananchi waiamini tena CCM kwa kumchagua Rais Magufuli kutokana na jitihada alizofanya katika kipindi cha miaka mitano iliopita cha kudhibiti wizi ,rushwa na ufisadi serikalini pamoja nakulinda rasilimali za nchi.
Ombi hilo amelitoa wakati wa mikutano yake ya kutafuta kura za ndio kwa wagombea wa CCM katika Kijiji cha Kwampunda na Kwamzuza vilivyopo kata ya usambara jimboni Bumbuli.
Alisema kuwa Mgombea wa CCM ambaye anamaliza kipindi chake cha awamu ya kwanza ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani licha ya kufanya mambo mengi ya kimaendeleo lakini pia amefanikiwa pia kurudisha nidhamu katika utumishi wa umma na kurudisha chachu mpya ya Watanzania ya kujitafutia Maendeleo.
” Ndugu zangu naomba muendelee kutuamini sisi CCM ili tuendelee kuwa tumikia kupunguza changamoto zilizobakia pamoja na kuendelea kukamata Ikulu ,Bunge na Halmashauri ya Bumbuli”alisema January Makamba ambaye kwa sasa ni Mbunge Mteule Wa Jimbo la Bumbuli.
Alisema kwa mujibu wa katiba ya nchi na utamaduni mamlaka ya kuchagua yapo kwa wananchi na ndio maana kila baada ya miaka mitano inatengenezwa ratiba ya vyama vyote kuja kuomba fursa na heshima ili kuomba ridhaa ya kuwatumikia tena katika kipindi kijacho.
Makamba alisema October 28 ndiyo siku iliyopangwa ili wananchi wa Tanzania waamue chama gani na wagombea gani wawaamini tena katika ngazi zote si jambo dogo na kwamba Duniani kote kunapofanyika uchaguzi ni jambo kubwa na zito na nchi inasimama.
Kwa maana hiyo amewaomba wanaBumbuli wasifanye makosa bali wachague mafiga matatu ya CCM ili wapate Maendeleo ya haraka.
Alisisiza kuwa Chama cha mapinduzi kimefanya mengi na kimetekeleza kwa kiasi kikubwa ahadi nyingi walizoahidi 2015 japo bado changamoto zipo lakini asipite mtu kuwadanganya kwamba atamaliza changamoto zote kwani tangu Dunia iumbwe hakuna mtu aliyewahi kumaliza changamoto zote.
Hata hivyo Makamba alisisitiza kuwa Rais Magufuli ameijengea heshima Tanzania na ,jumuia ya kimataifa na kwamba.
” Tumchague tena ili amalizie kazi aliyoianza kwani miaka mitano ya kwanza alikuwa anatengeneza mazingira mazuri lakini matunda yake tutayaona miaka mitano hii inayokuja “alisema Makamba.