***********************************
Na John Walter- Babati
Mabingwa wa kihistoria katika soka Tanzania, Yanga Sc wameichapa bao 5-4 Simba Sc katika mchezo wa kirafiki kati ya mashabiki wa timu hizo Mbili Babati mkaoni Manyara uliopigwa Uwanja wa Kwaraa mjini Babati.
Katika mchezo huo wa kirafiki uliovuta hisia za mashabiki wengi wa mpira wa miguu, katika dakika 90 za mchezo walitoshana Nguvu ya kufungana 1-1 Yanga wakitangulia kupata bao kipindi cha kwanza.
Kwa kuwa ilikuwa lazima mshindi apatikane,Mwamuzi wa mchezo huo Leo Oktoba 3,2020 alilazimika kuamuru mikwaju ya Penati.
Katika Mikwaju hiyo, Simba walipata Mikwaju 4 huku wakipoteza miwili hatua iliyowapa Yanga Ushindi kwa kuibuka na Mikwaju 5.
Mchezo huo maalum uliandaliwa na Babati Fitness Club (BFC) ambayo inaunda timu ya Simba na Yanga kwa upande wa Mashabiki kwa lengo la kuhamasusha wananchi kujitokeza kupiga kura kumchagua Rais, Mbunge na Diwani ifikapo Oktoba 28 mwaka huu.