Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta akishangilia baada ya kufunga mabao ya timu yake, Fenerbahçe katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Fatih Karagumruk kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Uturuki leo
…………………………………………………………………………….
Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanznaia ”TaifaStars” Mbwana Samatta leo ameifungia mabao mawili timu yake ya Fenerbahce katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fatih Karagumruk kwenye ligi kuu ya nchini Uturuki.
Hiyo ni mechi ya pili kwa Samatta kwenye ligi hiyo ambapo amecheza kwa dakika 84 kabla ya kufanyiwa mabadiliko.
Mechi yake ya kwanza ilikuwa ni dhidi ya Galatasaray wiki iliyopita ambapo alicheza kwa dakika 25 mechi ikimalizika kwa suluhu.