Afisa Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Maji Bi. Mwajuma Lugendo (kulia) akiwa na baadhi ya wakazi wa Kibaoni, mjini Mpanda akiwapa maelezo ya msingi kuhusu ushiriki wa jamii katika kuhakikisha uendelevu wa miradi ya maji na huduma ya maji katika makazi yao.
Tanki la kuhifadhi maji likiwa limekamilika ambapo maeneo yalikyokuwa na uhaba wa maji Mjini Mpanda yatapata huduma hiyo kwa saa 24. Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Mpanda (MUWASA) imesimamia kazi hiyo ambapo hali ya upatikanaji majisafi, salama na yenye kutosheleza kwa wananchi ikiwa ni matokeo ya uwekezaji katika sekta ya maji imeimarishwa.
Mkurugenzi Msaidizi, Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Maji Bw. Alex Tarimo (katikati), pamoja na wataalam wa sekta ya maji wakiangalia baadhi ya maeneo ambayo yatafikiwa na mtandao wa majisafi baada ya upanuzi wa mtandao na tanki la kuhifadhi maji kukamilika mjini Mpanda.
Jicho la ndege, taswira kutoka juu ya baadhi ya viunga vya mji wa Mpanda ambapo wakazi wake watapata huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza kwa saa 24. Hali ya upatikanaji maji kwa wananchi mjini Mpanda imeimarishwa na imepanda kutoka asilimia 8 ya mwaka 2016 hadi kufikia asiimia 75 mwaka 2020.