Mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini CCM, Anthony Mavunde Akizungumza na wajasiriamali wa Soko la Mnadani, Msalato jijini Dodoma alipofika kufanya manunuzi yake na kuzungumza na wajasiriamali hao.
Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma CCM, Mariam Ditopile akigawa vipeperushi vya Chama cha Mapinduzi kwa wajasiriamali wa Soko la Mnadani katika eneo la Msalato jijini Dodoma, Ditopile ameongozana na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde.
Msanii wa Bongo Fleva, Malaika akisalimiana na wananchi wa Jiji la Dodoma alipotembelea eneo la Mnadani Msalato ambapo aliambatana na Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo CCM, Anthony Mavunde na Mgombea Ubunge Viti Maalum Wanawake wa Mkoa huo, Mariam Ditopile.
…………………………………………………………………………..
Mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini CCM, Anthony Mavunde, na wa Viti Maalum Wanawake, Mariam Ditopile wakiambatana na Msanii Malaika wamefika katika eneo la Mnadani Msalato kusaka kura za Mgombea Urais, John Magufuli, Mbunge na Madiwani wa chama hicho ambapo wamegawa vipeperushi wa chama hicho na kufanya manunuzi yao binafsi.
” Watu wa Msalato leo mnafanya biashara zenu bila kusumbuliwa hii yote ni kwa sababu Dk Magufuli ameweka mazingira mazuri kwenu, gharama ambazo mlikua mnalipa mwanzoni zilikua kubwa sana lakini Rais Magufuli kwa kujali wanyonye akasema mtalipa 20,000 tu kwa mwaka mzima,” Ditopile.
” Kijana wenu nimekuja kwenu kuwashukuru kwa kuniamini kama Mbunge wenu kwa miaka mitano iliyopita, leo naomba tena nafasi niwatumikie kwa nguvu zaidi kuliko mwanzo, tujenge mtandao wa lami zaidi kuliko mwanzo, tuboreshe sekta ya Afya na zaidi tuweke mazingira yenu ya biashara katika ubora zaidi,” Mavunde.